Karibu Tawala (w)Longido Kamana Simba: katika Maalaigwanani wilaya ya Longido mmefanya tukio la kubariki elimu katika shule ya Kimokouwa pamoja na kuwaaga wanafunzi wa wanaotarajiwa kufanya mitihani ya kumaliza Elimu yao ya msingi,naomba Jambo hili lifanyike kila shule wilayani humu.

Laigwanani mkuuu Kiloriti Ole Ngulupa Tarafa ya Longido ambae ni pia ni mwasisi wa maombi ya kutengua mila na laana ambayo ilikuwa inawazuia watoto kwenda shule kusoma,pia amewahi kuwa diwani wa kata ya Kimokouwa kwa zaidi ya miaka 25
Muwakilishi wa Maalegwani (W) Salimu Alais:Elimu ni muhimu pamoja na Mimi kuwa kiongozi changamoto inayonipata ni pale kunapokuwa na nyaraka za kuandika siwezi kwasababu sijui kusoma Wala kuandika.


Mwalimu mkuu wa shule ya msingi Kimokouwa Thobias Minja: Watoto wa kike wakiendelezwa kielimu unapanua wigo mkubwa katika jamii.

Mwenyekiti wa shule ya msingi Kimwokouwa Laigwanani Saruma ole Kukuu,kukatisha masomo ya mwanafunzi ni kosa hatua za kisheria zichukuliwe kuondoa tatizo hili.

Na Vero Ignatus,Longido


Wazee wa Kimila Malaigwanani wilaya ya Longido wamefanya tukio la kubariki elimu katika shule ya Kimokouwa pamoja na kuwaaga wanafunzi wa wanaotarajiwa kufanya mitihani ya kumaliza Elimu yao ya msingi Septemba 8-9 ambapo tukio hilo linatambulika Kama EMAYANI ENG'ENO.

Akizungumza Katibu Tawala Kamana Simba kwa niaba ya mkuu wa wilaya ya Longido, aliwapongeza wazee hao kwa Jambo hilo walilolifanya, na kusema kuwa ni kubwa na linathamani hivyo amewaomba lifanyike katika wilaya nzima.

Simba aliwasisitiza Wazazi/walezi kuhakikisha wanahamasisha umuhimu wa Elimu kwa watoto wao, Sambamba na kuwataka wanafunzi kuzingatia Elimu,na kuishika kwani ndio msingi imara wa maisha yao ya baadae.

Aidha aliwataka waalimu kutokukata tamaa,kwani Serikali inatambua changamoto mbalimbali wanazozipitia pamoja na kufanya kazi katika mazingira magumu.

Kwa upande wake Laigwanani mkuu Kiloriti Ole Ngulupa, alisema kuwa elimu ni bora kwa watoto wote wa kike n awa kiume kuliko kitu kingine chochote katika maisha yao,hivyo Ni kosa kisheria kumkatisha mwanafunzi masomo yake kwani unamnyima haki yake ya msingi,na ikibainika hivyo Sheria ifuate mkondo wake.

Kiloriti Alisema jamii ya wafugaji iliyopo katika wilaya ya Longido, imefanya sala kwaajili ya kuwabariki watoto hao kwania ya kuwaombea juu ya mitihani yao wa mwisho unayofanyika tar 8-9 -2021 kwaajili ya kuhitimu elimu yao ya darasa la saba.

‘’Hivyo kwa sala hii tumewabariki watoto wa kila Kijiji ,tunamshukuru Munu jambo hili liwe la wilaya nzima sisi tumeamua kuwabariki watoto weetu kwa baraka ya mila nzuri kwasabababu tunahitaji elimu kwa watoto hawa,japokuwa matarajio ya mzanapompeleka mtoto shule yanakuwa makubwa ,pengine pale Watoto wetu hawajasoma kama tunatarajiaAmesema kuwa watoto wao baadhi yao wetu wanaishia darasa la saba, wengine akifika sekondari anaanza kidato cha kwanza anaishia kidato cha pili au cha tatu ,wanatoroka kenda nchi jirani,na wale ambao wanabahatika kwenda vyuoni wengi wao wanakosa ajira

Akisoma risala kwa mgeni rasmi mwalimu mkuu wa shule ya Kimokouwa ,Minja alisema shule hiyo yenye jumla ya wanafunzi 523 ambapo wavulana 257,wasicha 266,waalimu 10 wanaume 2wanawake 8 wapishi 2 na mlinzi 1 imekuwa ikifanya vizuri kitaaluma na imekuwa nafsi ya kumi bora kiwilaya.

"Hayo yanatokana nanjuhudi kubwa zinazofanywa na serikali yetu ikishirikiana na Wazazi,walezi,waalimu,pamoja na wanafunzi wa shule ya msingi Kimokouwa"Alisema Minja.

Aidha Minja alisema kuwa pamoja na mafanikio yote hayo ,zipo changamoto zinazo ikabili shule hiyo ikiwemo uzio eneo shule,shule kupatiwa hatimiliki tofauti na alama tu (bevons)ukarabati wa thamani na miundo mbinu chakavu,uhitaji mkubwa wa vifaa vya kufundishia na kujifunzia.

Changamoto nyingine ni pamoja na mwamko duni wawazazi kuchangia chakula kwa wanafunzi, upungufu wa mashime ya photokopi,thamani za ofisi za waalimu pamoja na upungufu wa matundu ya vyoo vya wanafunzi na waalimu.

"Watoto hawa wakiendelezwa kielimu wanauwezo mkubwa Sana,hivyo bado mtoto wa kike anayo nafasi kubwa Sana katika jamii yetu,Unapomwelimisha mtoto wa kike unapanua wigo mkubwa kwani unaelimisha jamii nzima"Alisema Minja.

Aidha shule ya msingi Kimokouwa ulianza rasmi mwaka 1978 ikiwa na jumla ya wanafunzi 23 wavulana 13 wasichana 10 waalimu 2 na vyumba 2 vya madarasa.

Hivi Sasa shule hiyo Ina jumla ya wanafunzi 523 ambapo wavulana Ni 257 wasichana 266,waalimu 10 ,wanawake 8 wanaume 2,wapishi 2 na mlinzi 1 na vyumba vya madarasa 9
Share To:

Post A Comment: