Na Atley Kuni-DODOMA


Naibu Waziri Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, anaye shughulikia Afya, Dkt. Festo Dugange, alihitimisha Mkutano Mkuu wa Mwaka wa Waganga Wakuu wa Mikoa na Halmashauri, huku akiwaachia kazi kubwa yakwenda kufanya ikiwepo Matumizi sahihi ya fedha zilizotolewa kwa ajili ya UVIKO-19 kutumika kwa malengo yaliyokusudiwa.


Akifunga Mkutano huo wa mwaka wa Mwaka wa Waganga wakuu wa Mikoa Pamoja na Halmashauri jijini Dodoma tarehe 16, Septemba, 2021, Dkt. Dugange alisema, serikali imetoa fedha kwaajili ya Mpango Shirikishi na Harakishi wa Jamii dhidi ya Chanjo ya Uviko-19, hivyo viongozi wa Mikoa na Halmashauri wanajukumu lakusimamia kwa umakini ili fedha hizo zitumike kwa malengo yaliyokusudiwa.


“Asitokee kiongozi yeyote kubadilisha matumizi ya fedha hizo” Alisisitiza Dkt. Dugange


Dkt. Dugange amewaambia Waganga wakuu hao kuwa Serikali inaendelea kupeleka fedha katika ujenzi wa vituo vya afya na katika hatua ya sasa, imepeleka bilioni 165.7 kwaajili ya ujenzi wa Hospitali 102, ukamilishaji wa maboma 555 na ujenzi wa vituo vya afya 71, ikiwa ni ukamilishaji wa bajeti ya 2020/21, na kuongeza kuwa kufikia Septemba 2021, jumla ya shilingi bilioni 37.5 zimepelekwa na serikali kwa ajili ya ujenzi wa Vituo vya afya kwenye tarafa 150 ambazo hazikuwa na vituo vya afya.


“Nichukue nafasi hii kuwaelekeza wakuu wa Mikoa, Wakuu wa Wilaya, Pamoja na nyie wataalam, mkasimamie kwa ukamilifu ili majengo hayo yakamilike kwa wakati na yaendane na thamani ya fedha iliyo pelekwa” ameelekeza Naibu Waziri Dugange.


Katika hatua nyingine, Dkt. Dugange amewataka viongozi hao, wakasimamie vema majukumu yao ili wananchi waridhishwe na kuvutiwa kupata huduma   katika vituo vya afya vya serikali kila wanapo zihitaji, kwani itasadia kuongeza mapato na kujiendesha vyenyewe,  lakini pia kuondosha rufaa zisizokuwa za lazima, huku akihimiza matumizi ya Mifumo ya TEHAMA yatakayo saidia kuwa na taarifa sahihi za kitakwimu kwenye Vituo vyote.


Awali kabla Dkt. Dugange kufunga mkutano huo, Waganga Wakuu wa Mikoa Pamoja na Halmashauri, walitoka na maazimio tisa, ikiwepo kufunga mitambo ya kuzalisha hewatiba ya oksijeni katika kila Hospitali ya Rufaa ya Mkoa na Halmashauri, kutekeleza Mpango wa Jamii Shirikishi na Harakishi Dhidi ya UVIKO-19 ili kuongeza kasi ya watu kuchanjwa.


Maazimio mengine ni ilikuwa kuhakikisha Kamati za Usimamizi katika ngazi za Mkoa na Halmashauri, kusimamia miradi ya ujenzi iliyopo katika maeneo yao, aidha Wakurugenzi wa Halmashauri waweze kutenga fedha za tathmini na ufuatiliaji wa miradi ya maendeleo kutoka kwenye vyanzo vya mapato ya ndani ya Halmashauri.


Viongozi hao walikubaliana pia vituo vipya vilivyojengwa vianze kutoa huduma kulingana na majengo yaliyokamilika kwakutumia vifaa na rasilimali   watu iliyopo hasa utoaji wa huduma ya wagonjwa wa nje na ile ya Mama na Mtoto (OPD, RCH, nk.)


Aidha fedha za miradi ya maendeleo zitumike kwa kuzingatia Sheria, Kanuni, Miongozo na Taratibu ili zisivuke mwaka wa fedha, vilevile wadau waliopo kushirikishwa ndani ya Mikoa na Halmashauri ili kuchangia bajeti za Mikoa na Halmashauri kila mwaka kulingana na vipaumbele vilivyopo, sula lingine walilokubaliana ni kuandaa Mwongozo wa Uchangiaji gharama za huduma za Damu Salama.


Na mwisho walikubaliana kuwa na Miongozo wa Ukaguzi wa Bidhaa za Afya utakaotumika kwenye vituo vya huduma za afya ngazi ya mikoa na Halmashauri Pamoja na kuhuisha Mwongozo wa Mshitiri uliopo sasa.


Awali akiendesha kikao hicho, Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais, Tawala za Miko ana Serikali za Mitaa, anayeshughulia Afya, Dkt. Grace Magembe, aliuambia Mkutano huo kuwa, ili kufanikiwa katika Mpango Jamii, Shirikishi na Harakishi wa Chanjo dhidi ya Uviko-19, nimuhimu kuwatumia wataalamu waliopo ngazi za Mikoa na Halmashauri kwakuwa wao wapo karibu zaidi na jamii.


Mkutano wa huo wa Siku tatu, uliandaliwa kwa ushirikiano wa Wizara ya Afya Pamoja na Ofisi ya Rais-TAMISEMI ambapo ulifunguliwa na Waziri wa Afya Dkt. Dorothy Gwajima na kufungwa na Naibu Waziri Ofisi ya Rais-TAMISEMI, huku ukiwa umebebwa na kaulimbiu, “Ustahamilivu wa Mifumo ya Afya katika Mapambano dhidi ua UVIKO-19 ‘Changamoto na Fursa’’.


MWISHO

Share To:

Post A Comment: