rais wa Chemba ya Wafanyabiashara, wenye viwanda na Kilimo Tanzania (TCCIA), Bw.Koyi Paul akikabidhi vyeti na leseni kwa wazalishaji ambao bidhaa zao zimekidhi ubora.hafla hiyo imefanyika leo Makao Makuu ya TBS Jijini Dar es Salaam.

rais wa Chemba ya Wafanyabiashara, wenye viwanda na Kilimo Tanzania (TCCIA), Bw.Koyi Paul akizungumza katika hafla ya utoaji leseni na vyeti vya ubora leo kwenye ofisi za TBS Makao Makuu Jijini Dar es Salaam.

Mkurugenzi wa Shirika la Viwnago Tanzania (TBS), Dkt.Athuman Ngenya akizungumza katika hafla ya utoaji leseni na vyeti vya ubora leo kwenye ofisi za TBS Makao Makuu Jijini Dar es Salaam. Mkurugenzi wa Udhibiti Ubora kutoka Shirika la Viwango Tanzania (TBS) Lazaro Msasalaga akizungumza katika hafla ya utoaji leseni na vyeti vya ubora leo kwenye ofisi za TBS Makao Makuu Jijini Dar es Salaam.

Wazalishaji wa bidhaa mbalimbali hapa nchini wakiwa katika hafla ya utoaji leseni na vyeti vya ubora leo kwenye ofisi za TBS Makao Makuu Jijini Dar es Salaam.

(PICHA ZOTE NA EMMANUEL MBATILO)

*****************************

NA EMMANUEL MBATILO, DAR ES SALAAM

Shirika la Viwango Tanzania (TBS) katika kipindi cha mwezi Mei hadi Septemba 2021, imeweza kutoa jumla ya leseni na vyeti 227 kwa wazalishaji ambao bidhaa zao zimethibitishwa kukidhi matakwa ya viwango.

Ameyasema hayo leo rais wa Chemba ya Wafanyabiashara, wenye viwanda na Kilimo Tanzania (TCCIA), Bw.Koyi Paul katika hafla ya utoaji leseni na vyeti vya ubora leo kwenye ofisi za TBS Makao Makuu Jijini Dar es Salaam.

Akizungumza katika hafla hiyo Bw.Paul amesema kati ya leseni na vyeti vilivyotolewa katika kipindi hicho, vyeti 105 sawa na asilimia 46.25% vilitolewa kwa wajasiriamali wadogo na wa kati.

"Leseni na vyeti vilivyotolewa vinahusisha bidhaa mbalimbali kama vile Chakula,Vipodozi,Viatu, Vifaa vya Ujenzi, Vifaa vya Umeme,Vifaa vya mitambo, Magodoro, vibebeo pamoja na vifungashio". Amesema Bw.Paul.

Amesema Serikali kupitia TBS imetumia Shilingi Milioni 715 kwa ajili ya kuwahudumia wajasiriamali wadogo na wa kati na utaratibu wa kuanza kulipa wao wenyewe umeshawekwa kupitia sera ya madeni ya shirika.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Shirika la Viwnago Tanzania (TBS), Dkt.Athuman Ngenya amesema leseni na vyeti ambavyo vimekabidhiwa kwa wazalishaji vitasaidia bidhaa zilizothibitishwa katika maeneo mbalimbali yakiwemo kuongeza imani kwa umma juu ya ubora, kupata faida ya kiushindani sokoni.

Amesema wazalishaji waliopewa vyeti na leseni ni wazalishaji wakubwa, wa kati pamoja na wajasiriamali wadogo.
Share To:

Post A Comment: