Mkuu wa Wilaya ya Lushoto ndugu Kalisti Lazaro amezindua mashindano ya "LUSHOTO TARAFA CUP" yenye Kauli mbiu "Cheza Salama, Ishi Salama, Funga Goli, Fungua Fursa & Kazi Iendelee" katika Uwanja  wa SEKOMU MAGAMBA kwa Timu za Magamba FC na Lushoto FC kucheza mechi ya Ufunguzi.


Mkuu wa Wilaya ya Lushoto aliambatana na Mwenyekiti wa Halmashauri wa Wilaya ya Lushoto ndugu Mathew P Mbaruku na Diwani wa Kata ya Lushoto Mjini ndugu Moka Urbani


Mashindano hayo yatajumuisha Kata Nane zilizopo katika Tarafa ya Lushoto; Kata za Lushoto, Ngulwi, Ubiri, Kwemashai, Gare, Kwai, Migambo na Magamba na kutakuwa na Makundi mawili ambapo Kundi la Kwanza litakuwa na Timu za Kwai, Migambo, Magamba na Gare na Mechi zitachezwa katika Uwanja wa SEKOMU MAGAMBA na Kundi la Pili lina Timu za Lushoto, Ubiri, Ngulwi na Kwemashai na Mechi zitachezwa katika Uwanja wa Hazina Lushoto.


Mshindi wa Kwanza atapata Zawadi ya Kombe, Jezi na Mpira, Mshindi wa Pili atapata Jezi na Mpira na Mshindi wa Tatu atapata Mpira.


Mashindano haya yanatarajia kuisha tarehe 14/10/2021 siku ya Nyerere Day na yamedhaminiwa na NMB Lushoto, Henken, Mazinde Juu Sekondari, LEVO, Halmashauri ya Wilaya ya Lushoto, Youth Development Ubiri na Azam Media.


Mkuu wa Wilaya ya Lushoto ndugu Kalisti Lazaro alitaka Mashindano hayo yawe endelevu na yasiendeshwe kwa mfumo wa Bonanza ili yasaidie kupatikana Timu moja ya Tarafa ya Lushoto ambapo baadaye Ofisi yake itadhamini Mashindano ya Wilaya kwa kushindanisha Tarafa zote Nane za Wilaya ya Lushoto.

Pia alisema " ... Nimesikia zawadi zilizotamkwa na Waandaaji wa Mashindano haya na kwa Ari niliyoina leo hapa Uwanjani ninahaaidi nitatoa kiasi cha Tsh 1,000,000/= kama nyoongeza ya zawadi kwa Washindi wa Mashindano haya.


Mkuu wa Wilaya ya Lushoto alitoa wito kwa Makatibu Tarafa na Wadau wengine wa Mpira wa Miguu kuandaa Ligi za Tarafa ili kila Tarafa itoe Timu moja katika Mashindano ya Wilaya yatakayodhaminiwa na Ofisi ya Mkuu wa Wilaya kwa kushirikiana na Wadau wengine wa Mpira wa Miguu na Kipekee aliwashukuru Waandaaji wa Mashindano wakiongozwa na Mwenyekiti wa Mashindano haya ya Lushoto Tarafa Cup Afisa Tarafa wa Tarafa ya Lushoto Bi Harriet Sutta na Afisa Michezo Halmashauri ya Wilaya ya Lushoto ndugu Keneth Gasper Makongo

Share To:

Post A Comment: