Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini IGP Simon Sirro amesema kwa kushirikiana na Jeshi la Polisi Nchini Rwanda wameazimia kwa moja kukabiliana na makosa yanayovuka mipaka ikiwemo makosa ya ugaidi kutokana na mkakati waliojiwekea mwezi Mei mwaka huu jijini Dar es salaam.

IGP Sirro amesema hayo jana muda mfupi baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa J. K. Nyerere jijini Dar es salaam wakati akitokea nchini Rwanda kwa ziara ya kikazi ya siku tatu iliyolenga kuboresha  ushirikiano wa matukio mbalimbali ya uhalifu na wahalifu.

Share To:

Post A Comment: