Mwanaume anayekadiriwa kuwa na umri wa miaka 42 amekutwa amefariki katika nyumba ya kulala wageni ya Uyowa katika Manispaa ya Tabora.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tabora Safia Jongo amesema tukio hilo limetokea usiku wa kuamkia Jumatano Septemba 8,2021 katika nyumba ya kulala wageni iliyopo jirani na Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Tabora Kitete.

Amesema chanzo cha kifo chake bado hakijajulikana na kwamba huenda siku zake zilikuwa zimefika akibainisha kuwa mtu anakufa mahali popote siku zake zikifika na huenda siku zake zilikuwa zimefika ingawa uchunguzi wa chanzo cha kifo chake kutoka kwa madaktari utaeleza chanzo
Share To:

Post A Comment: