Na. Angela Msimbira NJOMBE

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za  na Serikali za Mitaa Mhe Ummy Mwalimu  amesema  kuwa yeye ni waziri wa vijijini kwa kuwa  ndipo wananchi wanyonge walipo  na ndipo kero za owananchi zilipo zikiwemo kero za barabara, Maji, Elimu na afya

 Akiongea na wananchi wa kijiji cha Makowo katika kata ya Makowo, Mkoani Njombe leo wakati alipokuwa akikagua ujenzi wa Kituo cha afya cha Makowo Waziri Ummy amesema atatembelea maeneo ambayo hayafikiki kwa lengo la kutatua changamoto zao hasa kwenye maneneo ya vijijini ambapo ni mbali kufikika

“Maeneo ya pembezoni mwa miji hasa vijijini ndipo kwenye shida nyingi ambazo zinahitaji kutatuliwa, Nikiwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tamisemi nimebeba dhamana kubwa ya kutatua kero hizo na kuzitatua kwa wakati  lengo ni kuwasaidia wananchi wanyonge  na kuleta maendeleo kwa jamii.” Amesema Waziri Ummy 

Akijibu kero za wananhi wa Kata ya Makowo Waziri Ummy alitumia nafasi hiyo kuwapongeza wananchi hao   kwa kuibua mradi wa ujenzi wa Kituo cha afya  Makowo kwa kutumia nguvukazi na mali  katika ujenzi wa kituo hicho  kuunga mkono juhudi za serikali katika kuhakikisha wanachangia katika kuleta maendeleo ,hivyo  aliahidi kutoa kiasi cha shilingi milioni 300 kwa ajili ya ununuzu wa vifaa na vifaa tiba na gari la wagonjwa  ili kituo hicho kianze kutoa huduma kwa wananchi na kupunguza vifo vya wamama wajawazito wanaotembea umbali mrefu kufuata  huduma za afya.

Aidha, aliwapongeza Halmashauri yaMji wa Njombe kwa kutumia fdha za mapato ya ndani  kiasi cha shilingi milioni 500 kwa ajili ya ujenzi wa kituo hicho na kusema kuwa amefurahishwa kwa Halmashauri hiyo kutumia mapato hayo kutatua kero za wananchi na sio kutumika kwa ajili ya semina  na makongamano 

Amesema kuwa Fedha za Mapato ya Ndani kazi yake kubwa ni kutatua kero za wananchi, hivyo amewaagiza Wakurugenzi wote nchini kuhakikisha wanatenga fedha kwa ajili ya kutatua kero za wanannchi na miradi ya kimakakati ambayo inaleta tija kwa jamii 

Kwa upande wa ujenzi wa miundombinu ya barabara Waziri Ummy amesem Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassani amejikita  katika kuimarisha barabara za mijini na vijijini ambapo katika bajeti ya ujenzi wa miundombinu ya barabara imeongezeka kutoka  shilingi bilioni 8 kwa mwaka 2020/2021  hadi kufikioa  shilingi bilioni 19 kwa mwaka 2021/2022

Amefafanua kuwa  kwa upande  Halmashauri ya Mji wa Njombe  kwa mwaka wa fedha 2020/2021 haikuwa imepangiwa  fedha kwa ajili ya miradi ya maendeleo ya barabara lakini katika mwaka wa fedha 2021/2022 serikali imetenga kiasi cha shilingi biloni 4.3 lengo likiwa ni kuhakikisha barabara za vijijini zinafunguliwa.

Vilevile Waziri Ummy amesema Serikali itatoa kiasi cha shilingi cha shiliningi   bilioni 120 kwa ajili ya ujenzi wa Barabara kwa kiwango cha changarawe katika eneo la kijiji cha Makowa   ili iweze kupitika wakati wote lengo ni kubadilisha maisha ya wananchi wa vijijini 

Kwa upande wa elimu Waziri Ummy  amesema kuwa serikali imetenga kiasi cha shilingi milioni 12.5 boma moja kwa ajili ya ukamilishaji wa maboma hivyo amewaagiza wananchi kujiongeza  kwa kuchangia maendeleo ya ujenzi wa miundombinu ya Serikali ili kuunga mikono Serikali

Waziri Ummy yupo kwenye ziara ya kikazi katika Mkoa wa Njombe ambapo leo amekagua miradi ya maendeleo inayotekelezwa na Halmashauri ya Mji wa Njombe kwa kuweka  jiwe la msingi katika  Kituo cha afya Makowo, kuzindua  ujenzi wa Madarasa ya shule ya sekondari ya Matola na kukagua  ujenzi wa barabara  ya utalingolo

Share To:

Post A Comment: