Tume
ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), imelitangaza Jimbo la Konde huko Pemba kuwa
wazi baada ya mbunge mteule, Sheha Mpemba Faki kutangaza kujiuzulu
kabla ya kuapishwa na taratibu za kujaza nafasi hiyo zitatangazwa hivi
karibuni.
Taarifa iliyotolewa leo na Mkurugenzi wa Uchaguzi, Dk
Wilson Mahera imeeleza kuwa tume imepokea barua kutoka kwa Katibu Mkuu
wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Agosti 2 ikitoa taarifa kuwa mbunge huyo
mteule aliandika barua kwa chama chake kukitaarifu kuwa hayupo tayari
kuwawakilisha wananchi wa Konde katika Bunge la Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania kutokana na changamoto za kifamilia.



Post A Comment: