Mkuu wa Mkoa wa Pwani Aboubakar Kunenge akizungumza na Wananchi wa Vijiji vya Manda na Mkange Chalinze Wilayani Bagamoyo leo Agosti 3,2021.
 
Na Mwamvua Mwinyi,Pwani
MKUU wa Mkoa wa Pwani Aboubakar Kunenge amekutana na Wananchi wa Vijiji vya Manda na Mkange Chalinze Wilayani Bagamoyo, ambao wanalalamikia kutolipwa Fidia baada ya kuwepo Mchakato wa Ujenzi wa Barabara ya Afrika Mashariki, Makurunge, Saadani Tanga.

Kunenge ameeleza kuwa Awali Tathimini ya Fidia kwa Wanachi hao ilifanyika mwaka 2019 na malipo yamefanyika kwa Wananchi Pangani Tanga.

Jambo lilowatia hofu Wananchi hao ni kufanyika kwa Tathimini mpya ambayo fomula iliyotumika ni tofauti na ya mwaka 2019,hivyo kuwepo kwa Tathimini mbili kwenye mradi huo mmoja, na wakati huo huo Wananchi wa Vijiji Jirani wamelipwa kwa Tathimini ya awali.

"Mtalipwa Fidia kama walivyolipwa wenzenu wa Tanga, kwasababu ya Mazingira ya suala lenyewe kwamba Mradi ni mmoja Tathimini ilikwisha fanyika kilichofanya msilipwe kipindi hicho ni kukosekana kwa fedha" alisema Kunenge.

"Nimelichukua tutaenda kushauriana na Wizara fidia zilipwe kupitia vigezo walivyotumia kulipa wananchi wa Vijijini Jirani na kama inavyonekana kwenye Tathimini ya awali. Tutatumia hekima pia kutafutia ufumbuzi suala hilo alieleza Kunenge."vuteni subira suala hili tunalishughulikia"alisisitiza Kunenge.

Share To:

Post A Comment: