Mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya Kisarawe Mkoa wa pwani Hanan Mohammed Bafagil
RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan ameendelea
kuwaamini wanawake kwa kuwateua na kuwapa nafasi mbalimbali kwenye
Serikali yake ya Awamu ya Sita.
Agosti 2 mwaka huu, Rais
ametangaza wakurugenzi ambao watakwenda kutumikia majukumu yao kwenye
halmashauri mbalimbali na katika uteuzi huo wanawake wameendelea kupewa
nafasi ya kuaminiwa na Rais.
Miongoni mwa wanawake ambao wamepata
nafasi ya kuaminiwa na Rais Samia na kuteuliwa kushika nafasi ya
Ukurugenzi wa Halmashauri basi ni pamoja na Mkurugenzi wa Halmashauri ya
Wilaya ya Kisarawe mkoani Pwani Hanan Mohammed Bafagil.
Awali
katika Halmashauri ya Wilaya ya Kisarawe katika nafasi ya Ukurugenzi
alikuwa Mussa Gama ambaye sasa amehamishiwa Halmashauri ya Wilaya ya
Namtumbuka mkoani Ruvuma.Hanan kabla ya kuteuliwa kuwa Mkurugenzi
alikuwa Katibu Tawala wa Wilaya ya Arusha Mkoa wa Arusha.
Akizungumza
leo Agosti 3,2021, na Michuzi TV na Michuzi Blog Hanan amesema anatoa
shukrani kwa Rais Samia Suluhu Hassa kwa kumuani na kumteua kwenye
nafasi hiyo,hivyo atahakikisha anafanya kazi kwa bidii na maarifa yake
yote ili kuonesha imani yake kwa Rais na Watanzania hususan wananchi wa
Wilaya ya Kisarawe.
"Kuteuliwa kwangu na Rais kwenye nafasi hii ,
ninachoweza kwanza namshukuru Rais kwa imani yake kwangu lakini nieleze
huu ni mwendelezo tu wa kuendelea kupiga kazi , nimetoa Arusha na sasa
nimehamia Wilaya ya Kisarawe hakuna kulala nitaendelea kuungana na
wananchi kuhakikisha maendeleo katika wilaya yanapatikana,"amesema .
Aidha
amewaomba wananchi wa Wilaya hiyo kuonyesha ushirikiano katika kila
namna huku yeye akiahidi kuwa atashirikiana na wananchi pamoja wakuu
wote wa idara katika kufanikisha azma ya Serikali ya kupeleka maendeleo
kwa wananchi inatekelezwa kwa kasi.
Post A Comment: