Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Mhe. Omary Kipanga (mwenye kofia ya kijani) akifafanua jambo mara baada ya kukagua ujenzi wa jengo la madarasa na maabara linalojengwa katika Chuo cha Ufundi Arusha.


NAIBU Waziri wa Katiba na Sheria Geophrey Mizengo Pinda amevitaka vyuo vikuu nchini ambavyo vinatoa kozi ya mahakimu kuanza kubadili mfumo na kufundisha kwa lugha ya kiswahili ambayo wataitumia kazini baada ya kuhitimu kwa kuwa tayari Sheria ya kuendesha mashauri ya mahakama kwa lugha ya kiswahili imeshapitishwa.

Mizengo Pinda ametoa kauli hiyo jijini hapa jana wakati Akifungua mkutano wa wadau Kuhusu masuala ya msaada wa kisheria nna upatikanaji wa haki kwa wananchi iliyoandaliwa na wizara ya Katiba na sheria.

Amesema Sheria ya matumizi ya lugha hiyo ya kiswahili katika kuendesha mashauri imeshapitishwa hivyo mahakimu wahakikishe wanaitumia kikamilifu bila woga kwa lengo la kutoa haki kwa wananchi wakati wa kuendesha mashauri yao.

Naibu waziri huyo amesema suala la lugha limekuwa kikwazo kikubwa katika uendeshaji wa mashauri ambapo Wananchi wengi wamekuwa hawaelewi lugha hiyo hivyo kujikuta wakishindwa kuoata haki stahiki.

Amesema kwa sasa kuna haja ya vyuo vikuu nchini kubadili mfumo na kuanza kutumia lugha ya kiswahili kama lugha ya kufundishia kwa kuwa ndiyo lugha watakayokwenda kuitumia kazini baada ya kuhitimu masomo yao.

" Tunaka kwenda kwenye matumizi ya lugha yetu ya kiswahili katika uendeshaji w mashauri ambayo ni lugha mama na itakayorahisisha upatikanaji wa haki Mana lugha pekee imekuwa kikwazo kwenye upatikanaji wa haki," Amesema.

Alisema lugha hiyo mama ikitumika itawqsaidia watanzania kuelewa vyema tafsiri za masual ya kisheria, lakini wanapokutana na wageni basi mahakimu wananafasi ya kutumia lugha ya kigeni kuendesha mashauri yao.

"Usomi wetu watanzani hauwezi kutafsiriwa kwenye kutumika kwa watu ambao hawajui lugha ya kiswahili, mana hata tunapokwenda likizo kwa wazazi wetu lugha tunayotumia ni lugha yetu ya asili ili tuweze kuelewana ndicho tunachokitaka na huku,"alisisitiza naibu waziri.

Alitoa wito kwa washiriki kila mmoja kwa nafasi yake kutoa elimu juu ya masual hayo maana kutafsiri uendeshaji wa mashauri kwa lugha ya kiswahili katika uendeshaji wa mashauri ni jambo lingine na kujua watumiahi wanapokeaje na kwenda kuutumia lugha hiyo ambayo ni sehemu ya maboresho ni jambo lingine.

Akitoa mada Mkurugenzi Mtendaji Chama Cha Wanasheria Tanzania(TLS) Kaleb Gamaya akitoa mada Kuhusu msaada wa kisheria kwenye makosa ya jinai kwa amri ya mahakama, wigo, sifa za kupata huduma na upatikanaji wake. alisema kwenye mahakama pekee nchini watubwanaohitaji msaada wa kisheria ni wengi sana.

Gamanya alifafanua kuwa kwenye mahakama kuu zamani hakukuwa na msaada wa kisheria ila msaada huo ulikuwa ukitolewa kwa watuhumiwa wenye makosa mkubwa na ulikuwa ukitolewa kwenye makos mnne ikiwemo mauaji na uhaini, wigo wa msaada wa kisheria ulikuwa mdogo kipindi hicho tofauti na hivi sasa.

Pia alizungumzia idadi ndogo ya wakili ukilinganisha na idadi kubwa ya watuhumiwa waliopo jambo ambalo linawapa mzigo mkubw mawakili akiomba serikali kuelekeza fedha katika kukabiliana na idadi hiyo ndogo ya mawakili.
Share To:

Post A Comment: