Kundi
 la wadau wa maendeleo Mkoa wa Mara wanaoishi na kufanya kazi sehemu 
mbali mbali hapa nchini  (Mara Investors) limekabidhi jengo kwa ajili ya
 ofisi ya Serikali ya Mtaa ili kusaidia huduma za kiutawala kwa wakazi 
wa mtaa wa Serengeti Kata ya Nyatwali Bunda mjini.
Jengo
 hilo lenye thamani ya Shilingi 15.5  limejengwa kwa msaada wa wadau wa 
maendeleo wa mkoa Mara ikiwa ni Pamoja ,Dkt. Amon Manyama, Dkt. 
Sebastian Ndege na Wakili Deus Mgengeli.
Wadau
 hao wamejitolea kujenga ofisi hiyo ili kusaidia upatikanaji wa huduma 
za Kiserikali katika ngazi ya mtaa kutokana na mahitaji yanayokuwepo kwa
 Muda mrefu.Pia linatarajiwa kuwa kituo cha taarifa mbalimbali za 
kitalii na uwekezaji Katika eneo la Nyatwali,Bunda.
Akizungumza katika hafla fupi ya kukabidhi jengo hilo, Agosti 8,2021 Mkuu
 wa Wilaya ya Bunda Joshua Nasari aliwashuru wafadhili hao na kuwataka  
wakazi wa Bunda kupokea kwa mikono miwili ofisi hiyo na kujipanga kwa 
kumalizia kuongezea kile kilichopungua kwenye ofisi hiyo.
Nasari
 alisema ofisi hiyo itakuwa ni msaada mkubwa kwa kuwa Pamoja na kutoa 
huduma za kiserikali kwa wananchi wa eneo hilo, pia itatoa huduma ya 
taarifa za utalii hususani katika ukanda wa Magrabi mwa Serengeti.
Mkuu
 huyo wa wilaya aliwashukuru Mara Investors kwa kujitolea kujenga ofisi 
hiyo na kuwataka wadau wengine kujitokeza katika kusaidia jamii 
kupambana na changamoto mbali mbali ili kuweza kupata maendeleo.
"Sekta
 binafsi ni wadau wetu katika maendeleo ya nchi kwa ujumla,Serikali 
pekee haitoweza kufanikisha.Na nyie wananchi muunge mkono juhudi za 
serikali kwa kuchapa kazi,kupiga vita uzembe na tabia za umbea na 
uzururaji'',alisema Nassari.
Pamoja
 na kushiriki kuzindua ofisi hiyo Nassari  hiyo alipata fursa ya kupanda
 miti kadhaa ikiwa ni ni sehemu ya uhamasishaji wa kutunza mazingira 
wilayani humo.
Kwa
 upande wake, Dkt. Amon Manyama, mmoja wafadhili walichangia ujenzi 
,alisema yeye Pamoja na wenzake wamejipanga kwa ajili ya kusaidia  
kufikisha huduma ya maji na Umeme pamoja na miundombinu ya taa za 
kutumia umeme wa jua (solar) ili kuimarisha na kusaidia shughuli za 
kiuchumi na kijamii katika eneo la Ndabaka Centre.
Naye
 mwekezaji kutoka Jembe Group Dkt. Sebastian Ndege aliiomba serikali 
kuendelea kuweka mazingira mazuri kwa ajili ya kusaidia uwekezaji wenye 
tija unaofanywa na sekta binafsi.Aidha Dr Ndege aliahidi kuendelea 
kusaidia jitihada mbali mbali za kimaendeleo katika mtaa wa Serengeti 
kwa kufadhili Ujenzi  gati ya Maji safi na Salama na Choo cha Kisasa kwa
 ajili ya wageni na watalii wanaopita eneo hilo.Aidha amewataka uongozi 
wa Wilaya kunadili matumizi ya Soko lililojengwa hapo na kuwa 
gofu,litumike kama soko la kitalii ambapo litatoa ajira kwa vujana na 
kina mama wa Mtaa huo.
Mwekezaji
 mwingine kutoka Mara Investors Wakili Deogratius Mgengeli aliiomba 
serikali kushughulikia kero ya umiliki wa ardhi  kupitia Hati za kimila 
ili ziweze kutumika kupata mikopo ya uwekezaji katika eneo hilo.




Post A Comment: