
Naibu
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Khamis Hamza Chilo akizungumza na
wananchi wa Kijiji cha Paris kilichopo Wilaya ya Kati Mkoa wa Kusini
Unguja wakati wa mkutano wa hadhara uliofanyika leo ambapo amewataka
kutowaficha wahalifu wanaohatarisha usalama wao.Picha na Wizara ya Mambo
ya Ndani ya Nchi.
Na Abubakari Akida,MOHA
WANANCHI
wa kijiji cha Paris kilichopo Wilaya ya Kati Mkoa wa Kusini Unguja
Visiwani Zanzibar wametakiwa kutowaficha wahalifu wanaopatikana katika
maeneo yao ili kuweza kuishi kwa amani na salama ili lengo la nchi
kuendelea kiuchumi litimie.
Hayo
yamesemwa leo na Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Khamis Hamza
Chilo wakati akizungumza na wananchi wa Kijiji hicho kwenye Mkutano wa
Hadhara ambapo kabla ajazungumza nao alipata nafasi ya kusikiliza maoni
mbalimbali kutoka kwa wananchi hao.
Amewataka
wananchi hao kutoyafumbia macho matendo ya uhalifu ikiwemo uuzaji na
utumiaji wa dawa za kulevya,matendo ya udhalilishaji,uporaji na wizi
“Kuna
wengine wamesema yapo matukio ya kihalifu hapa yanafanyika, watu
wanaiba hapa, watu wanatembea uchi, bangi zinauzwa hapa, sasa akitokea
mtu anatokea sehemu ya mbali kama mlivyosema anafanya matendo ya
uhalifu basi mripoti kwa Jeshi la Polisi,mkishajua huyu ndio muuza unga
maarufu hata mimi niambieni nitawatauma askari wangu waje
wamshughulikie,msimpige wala msichukue sheria mkononi chukueni hatua za
kinidhamu na kisheria sio mumpige mtakuja kutengeneza balaa linguine”
alisema Naibu Waziri Chilo
Awali
mkazi wa Kijiji hicho Said Mpangaleni akizungumza katika mkutano huo
amesema kuwepo kwa uhalifu uliokithiri katika Kijiji chao imepelekea
kudumaa kwa shughuli za kimaendeleo watu wakihofia usalama wao
“Hapa
pana genge la uuzaji na utumiaji dawa za kulevya na ndio linaratibu
uhalifu wote katika Kijiji hiki,mtu akishakula maunga yake kinachofatia
ni uhalifu tu kwa kweli tumekua tukiishi kwa hofu,bora sisi wanaume tuna
afadhali lakini dada zetu wanaporwa mchana kweupe,serikali itusaidie
kwenye hili kwani kwa hali hii huo uchumi tunaoambiwa hatuwezi kuupata
hali huku ni tete” alisema Said
Wakitoa
neno la shukrani baada ya mkutano huo wawakilishi wa wananchi hao
wameiomba serikali kufungua kituo cha polisi katika maeneo hayo kwani
itarahisisha udhibiti wa uhalifu katika Kijiji chao hali itakayopelekea
kustawi kwa amani huku pia wakiomba kuongezwa kwa askari wa ulinzi
shirikishi.
Post A Comment: