Na Mwandishi wetu, Simanjiro

UONGOZI wa shule ya sekondari Mgutwa umewasaidia wanafunzi wa chekecheka, wa darasa la kwanza na la pili wa shule ya msingi Kandasikira Wilayani Simanjiro Mkoani Manyara, waliokuwa wanakaa sakafuni kwa kukosa madawati, kwa kuwakabidhi viti na meza hivyo kuondokana na kero hiyo.

Meneja wa shule ya sekondari ya Mgutwa, Monica Mlemeta amesema wametoa msaada huo ikiwemo kalamu na madaftari baada ya kubaini changamoto ya wanafunzi hao.Mlemeta amesema walitoa msaada wa viti 25, meza 25, vitabu, kalamu na vifuto ili kuwasaidia wanafunzi hao ambao wengi wao ni jamii ya watoto wa wafugaji waohamahama kila mara.

Amesema wazazi wengi na walezi wa wanafunzi hao wanaondoka na kuhama kufuata malisho ya mifugo yao hivyo wanawaacha wanafunzi hao kwenye wakati mgumu.Meneja huyo amesema shule ya sekondari Mgutwa ni majirani na shule hiyo ya msingi Kandasikira hivyo walipokuwa wanawatembelea walikuta tatizo hilo kwa wanafunzi hao.

Amesema wanamshukuru Mungu kwa hatua hiyo ila wanapaswa kuongeza msaada zaidi ikiwemo chakula, kwani wanafunzi hao wanatakiwa kula shuleni hivyo wasaidiwe. Amesema wanafunzi hao wanakabiliwa na changamoto ya kupata uji wa saa nne na chakula cha mchana, ili waweze kusoka kwa bidii hivyo wadau wa elimu wawasaidie hilo.

Amesema wanafunzi hao wanasoma kwenye vyumba vya madarasa yasiyo na sakafu chini, hivyo wanakaa kwenye madarasa yenye vumbi yanaymwagiwa maji ili wasome.
Share To:

Post A Comment: