Mbunge wa Jimbo la Dodoma Mjini Anthony Mavunde leo ameungana na wananchi wa kata ya Ihumwa Jijini Dodoma katika ujenzi wa kituo kipya cha Polisi na ujenzi wa vyumba vya madarasa ikiwa ni sehemu ya kuunga mkono juhudi za wananchi katika kujiletea maendeleo wenyewe.


Mbunge Mavunde ambaye ameshiriki katika uchimbaji wa msingi wa kituo cha Polisi ametumia fursa hiyo kuwataka wananchi kushirikiana pamoja kukamilisha ujenzi huo pamoja na ujenzi wa vyumba vya madarasa vya Shule mpya ya Ihumwa A,ambapo katika kuamsha ari ya michango miongoni mwa wananchi Mbunge huyo amechangia saruji mifuko 50 kwa kituo cha Polisi na nondo za 12mm za Tsh 2,000,000 kwa ajili ya ujenzi wa vyumba vya madarasa. 


“Nampongeza Diwani wenu Magawa,ameleta mapinduzi makubwa katika kutatua kero za wananchi ndani ya muda mfupi kwa kuishirikisha jamii.


Nami nitamuunga mkono kuhakikisha Kituo cha Polisi kinakamilika pamoja na ujenzi wa Shule mpya ya Msingi.Sisi tuanze kwanza na baadaye serikali itakuja kutuunga mkono”Alisema Mavunde


Akizungumza wakati wa zoezi hilo,Diwani wa kata ya Ihumwa Edward Magawa amemshukuru Mbunge Mavunde kwa kuwaunga mkono katika jitihada  anazoziongoza za kuwaletea wananchi wa Ihumwa maendeleo na kuahidi kusimamia misaada yote inatumika kwa malengo yaliyokusudiwa na kutumia fursa hiyo kuwaomba wananchi waendelee na moyo huo wa kujitolea ili kazi hizo za ujenzi zikamilike kwa wakati na wananchi wapate huduma stahiki.

Share To:

msumbanews

Post A Comment: