Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Maji Mhandisi Nadhifa Kemikimba akisikiliza maendeleo ya mradi mkubwa wa maji kutoka kwa Injinia Joilos Chilewa  ambapo ufikapo octoba 2021 utasambaza maji kwa sehemu kubwa katika Jiji la.Arusha .
Mhandisi Mshauri Mradi mkubwa wa maji Jiji la Arusha Injinia Joilos Chilewa akitoa ufafanuzi wa maendeleo ya mradi huo ambapo ufikapo octoba 2021utasambaza maji .
Baadhi ya timu iliyokuja kujifunza wakiongozwa na Katibu Mkuu Wizara ya Maji,Nishati na Madini wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ) Dk.Mngereza Mzee Miraji kuangalia namna ambavyo mradi huo umefanikiwa kwa kiasi kikubwa.
KATIBU Mkuu Wizara ya Maji,Nishati na Madini wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ) Dk.Mngereza Mzee Miraji na timu yake ya wizara wakiwa ziara ya  mafunzo katika mradi wa Sh.bilioni 520 wa  uboreshaji wa huduma za majisafi na Usafi wa Mazingira Arusha.
Fundi sanifu Maabara Ezekiel Mtema akionyesha namna ya kupima ubora wa maji AUWSA Jiji la Arusha.


Na.Vero Ignatus,Arusha

Mamlaka ya majisafi na usafi wa mazingira Jiji la Arusha (AUWSA),imetoa taarifa ya utekelezaji wa mradi unaogharimu sh.bilion 520, unaotekelezwa kwa mchango wa Serikali pamoja na mkopo kutoka Benki ya Maendeleo ya Afrika(AfDB) iliyowasilishwa kwa wajumbe kutoka Wizara ya maji ,Nisahati na Madini ya serikali ya mapinduzi ya Zanzibar.,   
Mratibu wa Mradi Mhandisi Gasto Mkawe, akisoma taarifa ya Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Jiji la Arusha (AUWSA) katika utekelezaji wa mradi wa kuboresha huduma ya majisafi na usafi wa Mazingira jijini humo na baadhi ya maeneo ya Wilaya ya Arumeru (ASUWSDP), alisema lengo la mradi huo ni  kuboresha hali ya upatikanaji wa majisafi na huduma ya uondoaji wa majitaka katika Jiji la Arusha ili kuboresha Afya na hali maisha ya wakazi wa Jiji kwa ujumla wake.

Akizungumza jana jijini Arusha mara baada ya kutembelea sehemu ya mradi huo, katika ujenzi wa Tanki la majisafi Seedfram  eneo la Ngaramtoni wilayani Arumeru,ujenzi wa ofisi ya Kanda Muriet  iliyopo jijini Arusha na mtambo wa kutibu majisafi, uliopo eneo la Midawe wilayani Arumeru,Katibu Mkuu Wizara ya Maji,Nishati na Madini wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ) Dkt.Mngereza Mzee Miraji alisema wametembelea mradi huo, ili kuona hatua waliyofikia na changamoto walizopata kwa ajili ya  wajifunze.

“Ziara hii ni utekelezaji wa maagizo ya Rais wetu ya kututaka tudumishe mahusiano  na tulianza  mchakato wake Februari mwaka huu wa  kuimarisha uhusiano  na kushirikiana kwa karibu katika utekelezaji wa miradi mbalimbali, ikiwa na kuandaa mpango kazi wa pamoja, lakini hata sisi itatusaidia kuboresha mradi wetu wa maji  wa Dola za Kimarekani milioni 92 tuliouanza utekelezaji wake,”alisema.

Aidha ziara hiyo licha ya kujifunza imelenga kudumisha ushirikiano kati ya serikali ya SMZ na Tanzania Bara, ili katika utekelezaji wa miradi ya maji uende sambamba pande zote za Muungano

Kwa upande wake Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Maji Mhandisi Nadhifa Kemikimba alisema ushirikiano huo, unalenga kuboresha maisha ya wananchi wa Tanzania Bara na Visiwani, ili kote kuwe na usawa   katika nyanja za maji na mengine.

“Maelekezo ya ushirikiano huo yapo toka mwaka 2010 ila sasa utekelezaji wake unaenda kasi zaidi na kuna manufaa kama wenzetu Zanzibar sehemu kubwa ya maji yao yanatoka chini ya ardhi hawana maji mtiririko, ila sisi Bara maji yetu yapo mtiririko kwenye mito,maporomoko ya maji na chini ya ardhi  kama katika mradi huu tunategemea visima 56 kutuleetea maji,mito na maeneo mengine,”alisema.

Alisema anaamini baada ya ziara hiyo wataenda kutekeleza mradi wao mkubwa waliouanza kutekeleza na lengo watakapotekeleza wasikwame sababu wameshafahamu changamoto na mafanikio tuliokutana nayo.

Aidha kutokana na kuongezeka kwa idadi ya wakazi wanaopata maji kutoka wastani wa watu 325,000 hadi kufikia wananchi 1,009,548,wameweza kuongeza matandao wa bomba za majisafi kutoka 44% hadi 100% ambapo jumla ya kilometa 545.7 za bomba mpya zitajengwa hii ni pamoja na kupunguza maji yanayopotea toka wastani wa 44%hadi 25%,ujenzi wa matanki 11 ya kuhifadhi majisafi yenye ukubwa wa jumla ya lita 45,500,000

Pia mradi huo umesaidi upatikanaji wa ajira kwa watu wapatao takribani 2,000 ikiwa ni watu 200 kutoka nje ya nchi ,ma 1800 kutoka ndani ya nchi kati ya 700 wakiwa wenye ujuzi mbalimbali.

Kutokana na mlipuko wa virusi vya korona (UVIKO-19) changamoto hiyo imeathiri upatikanaji wa vifaa vya ujenzi hasa vile vinavyoagizwa nje ya nchi na wataalam kutoka nje ya nchi ,kuchelewa  kwa upatikanaji wa msamaha wa kodi (GN)kwa wakandarasi na wataalam wasahauri,pamoja na uhaba wa vifaa vya ujenzi mfano sariji na malighafi ya utengenezaji wa bomba la chuma uliojitokeza mara kadhaa,kutokuwepo kwa maeneo yaliyotengwa na mipango miji kwaajili ya ujenzi wa miundombinu ya huduma za majisafi na majitaka.

Mara baada ya uwasilishaji wa ripoti iliambatana na ziara ya kutembelea ujenzi wa Tanki la majisafi Seedfarm Ngaramtoni,ujenzi wa Tanki la majisafi Burka,olasiti,ujenzi wa ofisi ya Kanda ,mtambowa kutibu majisafi midawi,ujenzi wa kituo cha kisukuma maji PS 03 maweni na ujenzi wa matanki ya majisafi Themi ,Themi Hill.
Share To:

Post A Comment: