Viongozi wa Umoja wa Wanafunzi wa Vyuo kutoka Jimbo la Kisesa wakiwa katika picha ya pamoja na Mbunge wa Jimbo la Kisesa, Mhe. Luhaga Mpina
Baadhi ya wanafunzi wa vyuo kutoka Jimbo la Kisesa wakiwa katika viwanja vya Bunge jijini Dodoma na Mbunge wa Kisesa, Mhe. Luhaga Mpina
Baadhi ya wanavyuo kutoka Jimbo la Kisesa wakiwa ndani ya ukumbi wa Bunge  wakifuatilia Hotuba ya Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto

Sehemu ya baadhi ya wanavyuo kutoka Jimbo la Kisesa wakifuatilia mjadala wa hotuba ya Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto bungeni Dodoma.
Baadhi ya wanafunzi wa vyuo kutoka Jimbo la Kisesa wakiwa katika picha ya pamoja na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk. Doroth Gwajima mara baada ya kuwasilisha hotuba yake bungeni Dodoma.  
 
Umoja wa Wanafunzi wa Vyuo Vikuu mbalimbali nchini wanaotoka Jimbo la Kisesa wamefika bungeni kujifunza namna Bunge linavyoendesha shughuli zake huku wakiahidi kusoma kwa bidii ili waweze kutoa mchango unaostahili kwa jimbo lao na Taifa kwa ujumla.

Mwenyekiti wa Umoja wa wanafunzi wa vyuo  kutoka Jimbo la Kisesa, Ndugu Sitta Kuzenza Nyangwakwa amesema umoja huo umeanzishwa kwa lengo la kuwakutanisha pamoja vijana wote wanaosoma vyuo mbalimbali kuanzia ngazi ya Diploma hadi Digrii wanaotoka Jimbo la KIsesa.

Amesema tayari wanafunzi wa vyuo wanaotoka Jimbo la Kisesa  kutoka Mikoa ya Dodoma, Morogoro, Dar es Salaam, Mbeya  wanaendelea kujiunga ili kuunga mkono juhudi za  Serikali pamoja na Mbunge wa Kisesa, Luhaga Mpina katika kuwaletea maendeleo ya jimbo hilo huku akitumia nafasi hiyo kuwahamasisha vijana wengine wanaotoka Jimbo la Kisesa kujiunga na umoja huo.
Baadhi ya wanafunzi wa vyuo kutoka Jimbo la Kisesa wakiwa katika viwanja vya Bunge na Mbunge wa Kisesa, Mhe. Luhaga Mpina
Share To:

TANGA RAHA BLOG

Post A Comment: