Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa,akizungumza wakati wa Mkutano wa uzinduzi wa ripoti ya tathmini ya utendaji kazi kwa Mamlaka za maji nchini iliyoandaliwa na Mamlaka ya Udhibiti wa Nishati na Maji (EWURA) na vitabu vya mwongozo wa uaandaji wa miradi ya maji kwa Wizara ya Maji iliyozinduliwa leo Mei 11,2021 jijini Dodoma.

Waziri wa Maji Mhe. Jumaa Aweso ,akizungumza wakati wa Mkutano wa uzinduzi ripoti ya tathmini ya utendaji kazi kwa Mamlaka za maji nchini iliyoandaliwa na Mamlaka ya Udhibiti wa Nishati na Maji (EWURA) na vitabu vya mwongozo wa uaandaji wa miradi ya maji kwa Wizara ya Maj iliyozinduliwa leo Mei 11,2021 jijini Dodoma.

Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa EWURA Mhandisi Godfrey Chibulunje akitoa taarifa kuhusu ripoti hiyo wakati wa uzinduzi ripoti ya tathmini ya utendaji kazi kwa Mamlaka za maji nchini iliyoandaliwa na Mamlaka ya Udhibiti wa Nishati na Maji (EWURA) na vitabu vya mwongozo wa uaandaji wa miradi ya maji kwa Wizara ya Maj iliyozinduliwa leo Mei 11,2021 jijini Dodoma.

Baadhi ya washiriki wa Mkutano wa Watendaji wa Sekta ya Maji wakimsikiliza,Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa (hayupo pichani) wakati wa uzinduzi wa ripoti ya tathmini ya utendaji kazi kwa Mamlaka za maji nchini iliyoandaliwa na Mamlaka ya Udhibiti wa Nishati na Maji (EWURA) na vitabu vya mwongozo wa uaandaji wa miradi ya maji kwa Wizara ya Maji iliyozinduliwa leo Mei 11,2021 jijini Dodoma.

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa,akiangali ripoti baada ya kukabidhiwa na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa EWURA Mhandisi Godfrey Chibulunje (wa mwisho kutoka kushoto) mara baada ya kuzindua ripoti ya tathmini ya utendaji kazi kwa Mamlaka za maji nchini iliyoandaliwa na Mamlaka ya Udhibiti wa Nishati na Maji (EWURA) na vitabu vya mwongozo wa uaandaji wa miradi ya maji kwa Wizara ya Maji iliyozinduliwa leo Mei 11,2021 jijini Dodoma.

Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa,akimkabidhi hundi Mwenyekiti wa Bodi Mhandisi Bashiri Mrinfoko wa tatu kushoto ( wa kwanza kushoto) ni Mkurugenzi Mhandisi Mgeyekwa baada ya Moshi kuibuka Mshindi wa Jumla wa Kwanza katika utendaji wa utoaji huduma yanmaji na usafi wa mazingira katika kundi la mamlaka za Miradi ya Kitaifa wakati wa uzinduzi ripoti ya tathmini ya utendaji kazi kwa Mamlaka za maji nchini iliyoandaliwa na Mamlaka ya Udhibiti wa Nishati na Maji (EWURA) na vitabu vya mwongozo wa uaandaji wa miradi ya maji kwa Wizara ya Maji iliyozinduliwa leo Mei 11,2021 jijini Dodoma.

Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa,akimkabidhi hundi Mwenyekiti wa Bodi wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Moshi Prof. Jafari Kideghesho Kushoto kwake ni Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maji Moshi, Mhandisi Kija Limbe baada ya Moshi kuibuka Mshindi wa Jumla wa Kwanza katika utendaji wa utoaji huduma ya maji na usafi wa mazingira katika kundi la mamlaka za maji za mikoa mara baada uzinduzi ripoti ya tathmini ya utendaji kazi kwa Mamlaka za maji nchini iliyoandaliwa na Mamlaka ya Udhibiti wa Nishati na Maji (EWURA) na vitabu vya mwongozo wa uaandaji wa miradi ya maji kwa Wizara ya Maji iliyozinduliwa leo Mei 11,2021 jijini Dodoma.

Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa,akikabidhi hundi Mwakilishi wa Mamlaka ya maji na usafi wa mazingira Biharamulo Bw.Mahmudu Bishanga kushoto kwake ni Mkurugenzi wa Mamlaka ya maji na usafi wa mazingira Biharamulo mara baada ya Biharamulo kuibuka mshindi wa kwanza katika utendaji wa utoaji huduma ya maji na usafi wa mazingira katika kundi la mamlaka za maji za Miradi ya kitaifa wakati wa uzinduzi ripoti ya tathmini ya utendaji kazi kwa Mamlaka za maji nchini iliyoandaliwa na Mamlaka ya Udhibiti wa Nishati na Maji (EWURA) na vitabu vya mwongozo wa uaandaji wa miradi ya maji kwa Wizara ya Maji iliyozinduliwa leo Mei 11,2021 jijini Dodoma.

...........................................................................................

Na.Alex Sonna,Dodoma

Mamlaka ya udhibiti wa huduma za nishati na maji hapa nchini UWURA leo Mei 11, 2021 imezindua ripoti ya tathmini ya hali ya utendaji kazi na utoaji huduma kwa mamlaka za maji hapa nchini ripoti inayolenga kuimarisha utoaji wa huduma za maji kwa wananchi.

Akizindua ripoti hiyo Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa amewataka watendaji katika mamlaka zote za maji ngazi zote hapa nchini kufanya kazi kwa kutanguliza uzalendo, uadilifu na weredi katika kazi zao.

Amesema Serikali imekuwa ikifanya kila jitihada kuhakikisha huduma ya maji inawafikia wananchi kama inavyotakiwa lakini kuna baadhi ya watendaji hawatimizi majukumu yao vizuri.

“Serikali inatumia fedha nyingi sana katika kutekeleza miradi lakini miradi hiyo haifanyi kazi kwa uzembe wa watendaji katika kusimamia miradi hiyo, nataka kila mmoja afanye kazi kwa weredi mkubwa ili wananchi wapate huduma za maji” amesema Mhe. Majaliwa.

Waziri Mkuu Majaliwa pia amezitaka mamlaka za maji kwenda kusimamia ipasavyo ukusanyaji wa ankara za maji ili kuwezesha mamlaka hizo kuendelea kujiendesha bila hasara huku zikizingatia sheria bila kuwabambikizia Ankara watumiaji wa maji kwani kuna malalamiko mengi sana.

Ameongeza kuwa “mkahamasishe watu kulipa ankara za maji na h ii sio kwa wananchi tu hata kwenye taasisi za serikali zote zilipe bili yeyote anayetumia maji lazima alipe ankara za maji mkasimamie hilo, pia tumepiga marufuku ukataji wa maji siku za wikendi au siku kuelekea wikendi” amesema.

Aidha ameitaka EWURA kwenda kusimamia uboreshwaji wa huduma za maji na kujenga utaratibu wa kufuatilia uboreshaji wa sera na kanuni katika kuhakikisha wananchi wanapata huduma bora za maji ipasavyo na kufuatilia tatizo la ucheleweshwaji wa miradi ya maji.

Awali, Waziri wa Maji Mhe. Jumaa Aweso amesema wao kama Wizara watahakikisha wanafanya kazi usiku na mchana kuhakikisha wananchi wanapata huduma bora za maji na hawatamvumilia mtu yeyote atakayekwenda na kutaka kurudisha nyuma jitihada hizo.

Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa EWURA Mhandisi Godfrey Chibulunje akitoa taarifa kuhusu ripoti hiyo amesema ripoti hiyo itasaidia katika kuimarisha utendaji kazi kwa Mamlaka zote na watakuwa wakitoa ripoti ya tathmini iliyofanyika ya utendaji wa kila Mamlaka katika mamlaka za Mikoa na miradi ya kitaifa na mamlaka za miji midogo na Wilaya.

Amesema wamefanya tathmini ya utendaji wa kila mamlaka na kupata Mamlaka zilizofanya vizuri katika kutoa huduma katika makundi ambapo kwa kundi la usimamizi wa miradi ya kitaifa aliyeibuka mshindi ni KASHWASA, Mamlaka za Mikoa ni Mamlaka ya Mkoa wa Moshi na Mamlaka za miji na Wilaya ni Bihalamuro ambazo zimezawadiwa shilingi milioni 21 kila mmoja ambazo watazitumia katika kununua dira za maji.

Share To:

TANGA RAHA BLOG

Post A Comment: