Katibu Mkuu wa TAMUFO, Stella Joel

Mlezi wa TAMUFO, Frank Richard 



Na Dotto Mwaibale

 

UMOJA wa Wanamuziki Tanzania  (TAMUFO) unaratajia kushiriki Maadhimisho ya Siku ya Makumbusho Duniani.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini hapa juzi Katibu Mkuu wa TAMUFO, Stella Joel alisema tayari wanamuziki kadhaa wameonesha nia ya kuadhimisha siku hiyo.

" Baadhi ya wanamuziki wameonesha nia ya kuhudhuria maadhimisho hayo ya makumbusho ya Taifa yatakayofanyika Mei 18, 2021." alisema Joel.

Mlezi wa TAMUFO, Frank Richard  alisema muziki ni sehemu katika Kuadhimisha  Siku ya Makumbusho  Duniani.

" Muziki ni wa muhimu sana hasa katika kipindi hiki ambacho tunahamasisha uanzishwaji wa makumbusho mbalimbali hapa nchini  zikiwemo za Wanamuziki kama mataifa mengine yaliyoendelea yanavyofanya.

Richard alisema  nchi nyingi duniani zina makumbusho mbalimbali zikiwemo za wanamuziki hivyo umefika wakati kwa  wanamuziki wa Tanzania kupata elimu kuhusu makumbusho ili waweze kuzianzisha chini ya taratibu na sheria za nchi.



































Share To:

Post A Comment:

Back To Top