Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Tarime (Vijijini), Simion K Damsel

Na Mwandishi wetu Mara,
MWENYEKITI wa Halmashauri ya Wilaya ya Tarime (Vijijini), Simion Samwel maarufu zaidi kwa jina la K, anashikiliwa na Jeshi lla Polisi Kanda Maalum ya Tarime-Rorya, kwa tuhuma za mauaji.

Uchunguzi uliofanywa na Mwandishi wetu aliyepo Mkoani Mara ubebaini kuwa K anashikiliwa tangu juzi, ingawa mpaka leo asubuhi Mei 19, 2021 jeshi hilo halijaweka hadharani tukio hilo.

K ambaye pia ni Diwani wa Kata ya Nyakonga wilayani Tarime, anatuhumiwa kuhusika katika mauaji ya Johnson Kagusa (30), yaliyotokea Mei 14, 2021 asubuhi mjini Tarime.

Inadaiwa kuwa saa chache kabla ya kufikwa na mauti hayo, kijana huyo alikamatwa na watu kadhaa siku hiyo saa moja asubuhi kwa tuhuma za kujaribu kuiba kwenye moja ya stoo ya bidhaa mjini Tarime. Habari hizi zimethibitishwa na Mwita Meck ambaye ni Mwenyekiti wa Mtaa wa Starehe alikokamatiwa kijana huyo.

Inaelezwa kwamba baada ya kukamatwa, kijana huyo hakupelekwa polisi, badala yake mwili wake uliokotwa na askari polisi baadaye siku hiyo hiyo saa saba mchana ukiwa umetelekezwa katika mtaa wa Posta na kupelekwa Hospitali ya Halmashauri ya Mji wa Tarime.

Taarifa tulizo nazo ninasema vyombo vya ulinzi na usalama ngazi ya wilaya vilifika hospitalini hapo kufuatilia na kuhakikisha hakuna upotoshaji wa majibu ya uchunguzi wa kubaini sababu ya kifo hicho.

Kaka wa Kagusa, Mwalimu Nelson Makoro ambaye ni Mkuu wa Shule ya Sekondari ya Rebu iliyopo mjini Tarime, amekiri kutokea kwa kifo hicho.

“Nimepoteza ndugu yangu, alikulia kwangu, tumemzika juzi Jumatatu wilayani Bunda,” Mwalimu Makolo

Hata hivyo, tangu K akamatwe kumekuwepo na jitihada za ‘udi na uvumba’ zinazofanywa na baadhi ya viongozi wa siasa akiwemo wa ngazi ya mkoa kujaribu kumnasua katika mkasa huo.

Viongozi hao wanakazania mpango wa ‘kumtoa ndani’ K huku wakitaka ikiwezekana jambo hilo limalizike kimya kimya, na wameonesha kutofurahishwa na waandishi wa habari wanaofuatilia tukio la kushikiliwa kwa mtuhumiwa huyo.
Share To:

msumbanews

Post A Comment: