Aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Singida, Dkt. Rehema Nchimbi (kulia)  akimkabidhi kabrasha  Mkuu wa Mkoa huo Mpya Dkt. Bilinith Mahenge katika hafla iliyofanyika ofisi ya mkuu wa mkoa mjini hapa.

Aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Singida, Dkt. Rehema Nchimbi (kulia), akizungumza katika hafla hiyo.

Hafla ikiendelea.


Katibu Mwenezi wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Singida, Ahmed Kaburu, akizungumza katika hafla hiyo.Viongozi wa Chama cha Mapinduzi (CCM)  Mkoa wa  Singida wakijitambulisha kwa mkuu wa mkoa mpya.
Wakuu wa Wilaya  Mkoa wa  Singida wakijitambulisha kwa mkuu wa mkoa mpya.
Viongozi wa dini  Mkoa wa  Singida wakijitambulisha kwa mkuu wa mkoa mpya.
Wenyeviti wa Halmashauri wakijitambulisha kwa mkuu wa mkoa mpya.
Wakurugenzi wa Halmashauri wakijitambulisha kwa mkuu wa mkoa mpya.

Hafla ikiendelea..
Hafla ikiendelea..


Hafla ikiendelea.


Picha ya pamoja na viongozi wa dini.
Na Dotto Mwaibale, Singida.


ALIYEKUWA Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt.Rehema Nchimbi ambae amestaafu utumishi wa umma amekabidhi ofisi kwa mkuu mpya wa mkoa huo Dkt.Binilith Mahenge ambapo amewashukuru watumishi wote wa mkoa huo kwa ushirikiano mkubwa waliompatia na kupelekea kustaafu kwa heshima.

Akizungumza katika hafla hiyo ya makabidhiano ya ofisi hiyo Dkt. Nchimbi limuomba Dkt. Mahenge kutumia uzoefu alionao kutoka makao makuu ya nchi kuisaidia na kuivuta Singida ili kuongeza kasi ya kuwaletea maendeleo wananchi wake kwa kuwa ni jirani na makao makuu ya nchi hasa kwa kuyaendeleza mazao ya Parachichi na Korosho.

Dkt. Mahenge akizungumza baada ya kukabidhiwa ofisi hiyo amewaomba ushirikiano watumishi wa ofisi hiyo kama walivyokuwa wakimpatia mtangulizi wake ili kuwatumikia wananchi wa mkoa kwa kuwaletea maendeleo.

"Jamani ninawaomba sana ushirikiano wenu kama mlivyoona hapa  mimi Mahenge nimeingia mimi kama mimi  sijaja na wale niliokuwa nafanya nao kazi,nyinyi ndio wenzangu hapa sasa." alisema Mahenge.

Aliwaomba watumie fursa hiyo kutafakari pale ambapo hawakufanya vizuri wakati wa Nchimbi kama ambavyo na yeye atatumia hiyo fursa kuongeza ufanisi wa utendaji wake wa kazi kama hakufanya vizuri wakati alipokuwa Dodoma.

Aidha aliwaahidi viongozi na wananchi wa mkoa huo kuyasimamia na kuyaendeleza yote yaliyoanzishwa na Dkt. Nchimbi hususani katika sekta ya kilimo ambapo amehamasisha kilimo cha Korosho na Parachichi,huku akitumia fursa hiyo kumshukuru Mh.Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kumuamini ili amsaidie katika mkoa huu.

Katibu Mwenezi wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Singida, Ahmed Kaburu alimwambi mkuu wa mkoa mpya kuwa Chama kitampa ushirikiano na kuwa kitaendelea kushirikiana na Serikali.

Makabidhiano hayo ya ofisi yamefanyika leo mbele ya viongozi wa mkoa huo akiwemo Katibu Tawala wa Mkoa, Wakuu wa Wilaya, Mstaki Meya, Viongozi wa Ulinzi na Usalama, Makatibu Tawala wa Wilaya na Wakuu wa Idara.

Share To:

Post A Comment: