Na Sharon Sauwa - Mwananchi
Watu wanaodaiwa kuwa wezi wameiba kikombe cha kuhifadhia ekaristi (Ciborium) kinachogharimu Sh5 milioni katika Kanisa Katoliki Parokia ya Mkoka wilayani Kongwa Mkoa wa Dodoma.

Mkuu wa Wilaya ya Kongwa, Dk Suleiman Serera ameieleza Mwananchi Digital leo Jumapili Machi 7, 2021 kuwa tukio hilo limetokea usiku wa kuamkia Jumapili Februari 28 2021.

Dk Serera amesema wezi hao walifungua mlango wa kanisa na kuchukua kikombe hicho na kisha kutokomea kusikojulikana.

“Polisi walimhoji Paroko akasema kuwa alifunga mlango. Bado wanaendelea na uchunguzi wa tukio hilo na hakuna aliyekamatwa,” amesema Serera ambaye ni mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama ya wilaya hiyo.

Amesema mazingira ya tukio hilo yanaonyesha kuwa ni mchongo kwa sababu wezi hao walichukua kikombe hicho tu na kuacha spika na kinanda kilichokuwepo ndani ya kanisa hilo.
Share To:

Post A Comment: