WAZIRI wa Maji Jumaa Aweso akichimba Mtaro wa Maji Mtaa wa Kiruku Kata ya Mabokweni Jijini Tanga hivi karibuni wakati wa ziara yake ya siku moja

Picha ikionyesha Bwawa la Mabayani na Sehemu ya Mto Zigi ambalo ndio chanzo cha Maji Jijini Tanga
Picha inaonyesha Mradi wa Maji Muheza ambapo hilo ni  tanki na kituo cha kusukuma maji kutoka  eneo la Kilapura Jijini Tanga hadi wilayani Muheza
Picha zinaonyesha eneo la mtambo wa kutibu maji Mowe

Ujenzi wa Manhole Chamber kwenye Mradi wa Maji Taka wa Duga Mwembeni Jijini Tanga

IKIWA ni siku chache kabla ya kuelekea maadhimisho ya wiki ya Maji Duniani inayotarajiwa kufanyika kuanzia Machi 16 hadi 22 mwaka huu hapa nchini mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Tanga Uwasa imefanikiwa kutekeleza miradi mikubwa sita ambayo itasaidia kuondosha tatizo la maji.

Hatua hiyo inatajwa kwamba itasaidia wananchi ambao walikuwa wakikumbana na adha ya kusaka maji na kushindwa kujikita kwenye shughuli za kimaendeleo kutokana na changamoto hiyo na hivyo kujikita kwenye uzalishaji na shughuli za kila siku na hivyo kujikwamua kiuchumi.

Miradi hiyo inatajwa kwamba itawawezesha pia kuongeza uzalishaji wa huduma ya maji iliyokuwepo awali katika maeneo husika na hivyo kupelekea huduma hiyo muhimu kwa jamii wa mijini na vijijini katika utekelezaji wa shughuli zao za kila siku

Akizungumza na Mwandishi wa Makala hii namna mamlaka hiyo iliyojipanga Mhandisi wa Mipango na Ujenzi Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Tanga Uwasa,Mhandisi Salum Ngumbi anasema ili kuhakikisha hayo yote yanakwisha wamepanga kutekeleza miradi mikubwa sita kwa mwaka huu wa Fedha wa kuboresha huduma ya maji Tanga kama ifuatavyo;

1.       Mradi wa kuboresha huduma ya maji Jijini Tanga Awamu ya Pili (Phase II)

Anasema kwamba awamu hii ina lengo la kutaka kuongeza kiasi cha maji kwenye Jiji la Tanga na wilaya ya Muheza ambapo kwa sasa mitambo yao ya kutibu na kusafisha maji ina uwezo wa kusafisha na kutibu maji mita za ujazo 30,000 kwa siku hivyo mradi huo utaongeza uzalishaji wa maji kwenye vituo vyao vya kutibu maji kutoka mita hizo za ujazo elfu 30000 kwa siku hadi kufikia 45,000 ambapo utakapomalizika utaondoa matatizo yanayowakabili wananchi wa Tanga mjini na Muheza.

“Kwa maana hasa wakati wa mchana kuna kuwa na presha ndogo ya maji kutokana na kuzalisha kiasi kidogo wakati Jiji la Tanga likiendelea kukua kutokana na uwekezaji mkubwa unaofanywa na serikali hivyo kuna ongezeko la watu sana na sisi ndio wenye jukumu hilo na ndio maana  tukabuni mradi huo”Alisema

Anasema waliamua kubuni mradi huo ili kuhakikisha wanakwenda sambamba na azma ya Rais Dkt John Magufuli kuhakikisha nchi inakuwa kwenye uchumi wa Kati ambapo mradi huo utakuwa na gharama za Bilioni 8.4 ambao unatekeleza na Tanga Uwasa kupitia fedha za Mkopo kutoka Benki ya TIB.

“Mradi huu utakuwa na kazi kama nne kubwa kukarabati mtambo wa kutibu maji Mowe,miundombinu iliyopo ikiwemo kutanua mtambo na kuongeza machujio mawili na clarifaya moja na hizo zote zitasababisha ongezeko la mita za ujazo elfu 15000 kwa siku”Alisema

Mhandisi Salum anasema pia watajenga tenki jengine kubwa la kuhifadhi Maji eneo la Mowe ambapo sasa hivi wana tenki la mita za ujazo 1,000,000 na watajenga jingine la pili lenye mita za ujazo 1,000,000 ili kukidhi mahitaji ya maji eneo la mjini ikiwemo kujenga bomba kubwa lenye urefu wa kilimota 12.5  kutoka Mowe hadi eneo la Matenki Kange Jeshini.

Anasema bomba hilo litakuwa na kipenyo cha Milimita 600 na  hivi sasa wana bomba lengine lenye milimita 600 hivyo wanaongeza la pili ili kuhakikisha maji wanayosafishwa na kutibiwa mowe yanawafikia wananchi kwa wakati  ambapo mradi huo utaanza mwezi Aprili mwaka huu na utakuwa na miezi 12 na utasimamia na wahandisi na wataalamu wengine kutoka Tanga.Uwasa .

2.       Mradi wa Uboreshaji Huduma Ya Maji Mji wa Muheza

Mhandisi Salum anaeleza pia mradi wa Pili utakuwa ni mradi mkubwa utakao toa maji kutoka chanzo cha Mabayani na Mtambo wa kutibu Maji eneo la  Mowe na utamaliza tatizo la maji Muheza kufikia asilimia 64 mradi huo utakuwa ni wa kuboresha huduma ya maji mji wa Muheza ambapo utakapokamilika utasaidia kunufaisha wakazi wa Muheza 15,000 na wakazi wa Vijiji vya Jirani mradi huo unapopita.

“Maeneo hayo ni Kilapura ,Kitisa na Lusanga vitanufaika na mradi huo ulianza mwaka 2019 na hadi kufikia sasa umefikia asilimia 90 vitu ambavyo vilipangwa kufanyika kwenye mradi huo ni kulaza bomba lenye urefu wa kilomita 21.6 kutokea chanzo cha Maji Mowe hadi kwenye Kijiji cha Kitisa”Anasema

Anasisitiza kwamba wataunganisha na bomba lililopo ambalo likalofikisha maji mji wa Muheza kwenye Matenki ya NHC ambapo mradi huo umeshaanza kutoa huduma hiyo kwa kutumia bomba lililopo la Pongwe na kwamba wananchi wa Muheza wameunganishiwa kwa sababu kuna kipande cha kilomita 16.9 na pia mradi huo ulihusisha ujenzi wa Tenki la Lita laki saba (700,000)kwenye kijiji cha Kilapura na kituo cha kusukumia maji hivyo vyote vimeshakamilika na vimeanza kutoa huduma.

Anaeleza kwamba kipande ambacho kilichobakia ni kulaza bomba lenye urefu wa kilomita 8.2 na mpaka sasa wamekwisha kulaza kilomita 8 bado mita 200 na wanategemea mpaka mwishomi mwa mwezi Machi mwaka huu utakuwa umekamilika.

“Lakini kwa hivi sasa tunatoa huduma na wananchi wa Muheza wanapata maji kwa mgao kwa siku tatu kwa wiki Jumatatu,Jumatano na Ijumaa hivyo mradi huo utakapokamilika wananchi watapata huduma siku saba kwa wiki na kuondosha changamoto zilizopo “Anasema

3.       Mradi wa Kuendeleza Eneo la kutoa huduma ya maji Jijini Tanga (Line Extension)

Hata hivyo anaongeza kwa upande wa Jiji la Tanga wananchi wanaongezeka na kutanuka kutokana na wananchi wengi kujenga meneo ya pembezoni mwa mji hatua ambayo iliyopelekea wao kuanzisha mradi ambao wana ufadhili wenyewe Tanga Uwasa kwa gharamna ya shilingi milioni 320 wanatarajia kuongeza eneo la utoaji wa huduma kwa kilomoita 20 mkwa mwaka huu wa fedha 2021.

Anaeleza kwamba mradi huo umekwisha kuanza na utawanufaisha wananchi maeneo ya Kange Kasera Kange Mkurugenzi ,Pongwe,Neema,Mwakidila na Masiwani,Mwahako na mafundi  wao wapo  kwenye maeneo ya mradi na wanaendelea kulaza mabomba makubwa na  wanatarajia kuwaunganisha wateja wapatao 2000 mradi ambao wanautekeleza kupitia fedha za ndani ikiwemo kutumia vijana wa mtaani kuchimba mtaro na mafundi wao.

4.       Mradi wa Kukarabati Mtandao wa Maji katika Mji wa Pangani

Akizungumzia kuhusu wilaya ya Pangani,Mhandisi Salum anasema wana mradi wa kuongeza eneo la utoaji wa huduma kilomita 15 ambapo wametenga milioni 100 kwa ajili ya kufanya maboresho katika maeneo ya Boza,Mkalamo na Madanga maeneo yote yatanufaika na mradi huo ambao unatekelezwa kupita fedha za ndani watatumia wananchi na mafundi wao.

5.       Mradi wa Kukarabati na kuboresha Miundombinu ya Maji katika Mji wa Muheza Awamu ya Kwanza (Phase I).

Akielezea namna walivyojipanga kuhusu uboreshaji wa huduma ya maji Muheza kutoka asilimia 34 hadi 64 anaeleza baada ya kukabidhiwa wamegundua miundombinu iliyokuwepo awali ni chakavu na baadhi ya maeneo mtandao haujafika na waliandika andiko la kuboresha miundombinu mjini na walilipeleka wizarani.

Anasema baada ya kulipeleka Wizara iliwaagiza wafanye haraka watekeleze mradi huo na huo mradi una thamani ya Bilioni 4.8 lakini kwa awamu ya kwanza wataanza na gharama ya milioni 500 mpaka sasa  wanashukuru wizara ya maji  tayari wamekwisha kupokea milioni 300 kwa ajili ya kufanya ukarabati huo mradi na kuongeza eneo la kutolea huduma.

Mhandisi huyo anaeleza kwamba hivi sasa wapo kwenye hatua za manunuzi ya mabomba na viungishio vyake wanatarajia watavipata mwishoni mwa mwezi wa pili au mwanzoni mwa mwezi wa tatu hivyo watahakikisha wanakarabati maeneo ambayo mabomba yake ni chakavu kwa kutumia fedha za ndani kwa saabu hivi sasa wanapeleka maji kwa mgao.

“Lakini maji wengi yanamwagika mitaani kutokana na miundonbinu mibovu watakarabati kwa kutumia wataalamu wao wa ndani na vijana kuchimba mitaro na mradi huo utakamilika mwezi June mwaka huu na hivyo kuongeza wigo wa upatikanaji wa huduma hiyo muhimu”Anasema Mhandisi huyo.

6.       Mradi wa Majitaka Duga Mwembeni

Kuhusu Mradi mwengine wa kuondoa maji taka na kuyapeleka sehemu stahiki  ambayo sio hatarishi anasema wana mradi wa kujenga mradi wa majitaka kutoka eneo la Duga mwembeni hadi katika kituo cha kusukumia majitaka kilichopo eneo lao la Makorora .

Share To:

TANGA RAHA BLOG

Post A Comment: