Baadhi ya mifuko ya saruji iliyonunua na mbunge kwa fedha za mfuko wa jimbo inayotarajiwa kugawiwa katika kata na vijiji ili kusaidia ukamilishwaji wa miradi ya maendeleo.

Mbunge wa jimbo la Ludewa mkoani Njombe wakili Joseph Kamonga akizungumza na wajumbe wa kikao cha DCC pamoja na wadau wa elimu namna watakavyoendelea kupambana ili kuwaletea maendeleo wananchi wa jimbo hilo.

Dkt,Stanley Mlay Mganga mkuu wa halmashauri ya wilaya ya Ludewa akishukuru na kueleza namna vifaahivyo vitakavyosaidia utekelezwaji wa miradi katika sekta yake ya afya.Na Amiri Kilagalila,Njombe

Zaidi ya milioni 40 fedha kutoka mfuko wa jimbo la Ludewa mkoani Njombe,zimetumika awamu ya kwanza kwa ajili ya kununua mifuko ya saruji 1200 pamoja na bati 968 ili kusaidi ukamilishwaji wa maboma ya miradi ya afya na elimu iliyokwama kwa muda mrefu kwenye vijiji na kata jimboni humo.

Mbunge wa Jimbo la Ludewa mkoani Njombe wakili Joseph Kamonga kabla ya kukabidhi vifaa hivyo kwa madiwani na watendaji wa kata katika kikao cha wadau wa elimu kilichofanyika wilayani humo,amesema msaada huo umetolewa ili kusaidia majengo yaliyoanzishwa na wananchi na kukwama kwa muda mrefu angali wananchi wametokwa na jasho wakati wa kuanzishwa kwa miradi.

“Kuna baadhi ya majengo wananchi wamepaua kabisa lakini kuezeka bado, kwenye vijiji na kata wananchi wametoka jasho mpaka wamekuwa wazito kuendelea kuchangia”

Aliongeza “Tumekusanya takwimu kwa picha na jengo kila lilipo na tunaahidi kushughulikia jambo lolote ambalo lina manufaa kwa wananchi wetu bila kujali ni nani aliyelianzisha”aliongeza Kamonga

Aidha amesema ugawaji wa vifaa hivyo ni pamoja na utekelezwaji wa ahadi mbali mbali  ikiwemo za ukamilishwaji wa majengo hayo na kuwataka wanachi na kata ambazo hazijapata kwa awamu hii kuwa wavumilivu kwa kuwa imeangaliwa jingo lenye hatua nzuri.

Miradi mingi inayotarajiwa kunufaika na vifaa hivyo ni pamoja vituo vya afya na zahanati,Mganga mkuu wa halmashauri ya wilaya ya Ludewa Dkt,Stanley Mlay amesema halmashauri ina zahanati 18 na vituo vya afya 14 ambayo vipo katika hatua mbali mbali za ujenzi hivyo wanategemea kuongezeka kwa kasi ya ujenzi kupitia misaada hiyo.

“Lakini nitumie nafasi hii kuwashukuru wananchi ambao kwa kiasi kikubwa wamekuwa wakishiriki katika ujenzi wa vituo vya afya na zahanati nah ii inaonyesha ni jinsi gani wanauhitaji wa huduma za afya kusogezwa karibu,Pia nimpongeze sana Mbunge wa Ludewa kwa kuwa ametusaidia sana kuhakikisha wananchi wanapunguziwa mzigo kwenye ujenzi kwa kuwa vifaa hivi vitasogeza hatua za ujenzi”alisema Dkt,Mlay

Baadhi ya madiwani na watendaji wa kata akiwemo Vasco Mgimba diwani wa kata Ludende na Wilbad Mwinuka diwani wa kata ya Luana wameshukuru kwa msaada huo kutoka mfuko wa jimbo kwa kuwa utakuwa na msaada mkubwa kukamilisha maboma mbali mbali ya afya na elimu katika kata zao.


Share To:

Post A Comment: