Na Raheem Secha,Songwe
Shule ya msingi Ivwanga kata ya Mlowo, Wilayani Mbozi Mkoani Songwe mapema leo jumatatu asubuhi afisa Elimu wa Mkoa wa Juma Kaponda amefanya ziara ya kushitukiza shuleni hapo kuanzia mida ya saa 1:00 asubuhi ambapo amefanya hivyo ikiwa ni lengo la kuangalia ufanisi wa kazi wa waalimu wa shule hiyo na kuangalia maendeleo ya shule hiyo pamoja na changamoto zinazoikabili shule.
Kaimu Mkuu wa Shule Mwalimu Ana Shipela ndie aliempokea na kuanza ukaguzi wa darasa moja baada ya lingine kujionea hali halisi ya mazingira ya masomo kwa wanafunzi wa shule hiyo ambapo aliambata na maratibu wa Elimu kata Seliady Mbugi.
Akiwa shuleni hapo afisa Elimu amechukizwa na uchelewaji wa waalimu kufika eneo lao la kazi na amewataka kuacha hiyo tabia mara moja na kuwataka wawe na misingi ya taaluma zao na amewapongeza baadhi ya waalimu wanazingatia muda. Kaponda pia amesema anajua kuwa kuna changamoto za miundo mbinu katika ufundishaji hivyo amesema pamoja na changamoto zote wajitahidi kufundisha na kutumia mbinu walizofundishwa aidha amesikitika na kushuka kwa ufaulu wa wa shule hiyo ambapo mwaka 2018 walikuwa na asiliamia 95,mwaka 2019 asiliamia 93 na mwaka 2020 asiliamia 88 amesema ufauli wa namna hivyo haukubaliki katika taaluma hivyo waalimu wa shule hiyo wajipange.
Kaponda pia ametoa maagizo kwa shule kuhakikisha wanafanya ukarabati wa madarasa ya shule na kuwaeleza kuwa pesa wanazopewa na serikali sio pesa za Mwalimu Mkuu hivyo waalimu wote wanapaswa kupanga matumizi yakiwemo.ukarabati wa madarasa ya shule hiyo ambapo miundo mbinu yake imeonyesha wazi kumkera Afisa Elimu Mkoa.
Wakati huo huo mratibu kata Elimu Seliady Mbugi amemuonyesha Afisa Elimu Madawati 20 ambayo yanatengenezwa shuleni hapo ili kukabiliana na uhaba mkubwa wa madawati hali iliopelekea wanafunzi kuwepo ambao wanakuja asubuhi na wengine mchana lakini ameahidi kulimaliza tatizo hilo likiwemo la madarasa ambapo wameanza kumalizia madarasa mapya yalioanza kujengwa shuleni ili kupungunguza msongamano.
Shule hiyo ina wanafunzi zaidi ya 1800 na ina idadi ya madawati 260 tu.
Post A Comment: