NA HER SHAABAN


DIWANI wa Kata ya Kipawa Halmashauri ya Ilala, Aidani Kwezi amesema mikakati yake ya maendeleo katika kata hiyo ni kusimamia Mapato ya Manispaa ya Ilala. Diwani Aidani aliyasema hayo Dar es Salaam leo katika kikao cha Maendeleo kata wakati wa kuelezea mikakati yake ya Maendeleo. 


"Katika utekelezaji wa Ilani ya Chama cha Mapinduzi CCM mikakati yangu katika kata hii kipaumbele cha kwanza mpango kazi wangu  ni kutoa elimu kuhamasisha  wafanyabiashara kulipia leseni na vibali vinavyotakiwa kisheria sambamba na kulipa leseni za biashara "alisema Aidan


Diwani Aidani alisema pia kuimiza Wananchi na Wafanyabiashara kulipa kodi na tozo kwa maendeleo ya nchi.


Aidha pia kuwapatia Wajasiriamali wote vitamburisho vya biashara na kuandaa takwimu sahihi kulingana na makundi yao ya biashara. 


Pia kuanzisha magurio katika viwanja vya wazi ili kujikwamua kiuchumi wananchi wake pamoja na kusogeza huduma kwa wananchi pamoja na kuwawekea mazingira bora Wawekezaji ndani ya kata hiyo


Mikakati mingine alisema kuboresha kata hiyo kuwa ya kisasa ikiwemo kujenga masoko ya kisasa,urasimishaji wa Ardhi, kuboresha miundombinu ya kata hiyo.


Kuakikisha wananchi wake wanapata huduma za maji safi na salama,kuwakikisha Wananchi wanapatai mikopo ya Serikali isiyo na riba ambayo inatolewa ngazi ya Halmashauri ya asilimia kumi ya wanawake Vijana na Watu Wenye Ulemavu pamoja na kuboresha sekta ya elimu.Kwa upande wake Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa Mogo Geroge Mtambalike amependekeza Wakandarasi wa takataka wawe chini ya Kata wasiletwe na halmashauri. 


Mwenyekiti Mtambakike pia ameshauri Waziri wa Mazingira aunde mabaraza ya Kata ya Mazingira kwa ajili ya kusimamia mazingira ya kata husika.


Afisa Mtendaji wa Kipawa Adeltus Kazinduki amewataka Wenyeviti wa Serikali za Mitaa kufufua Kamati za Usafi na mazingira zote ili wasimamie usafi. 


Diwani wa Viti Maalum Wanawake Ilala Magreth Cheka alisema atashirikina na Diwani wa kata katika kuleta maendeleo pamoja na kuwasimamia Wanawake, Vijjana na Watu wenye Ulemavu Waunde vikundi visajiliwe waweze kupata mikopo ya Halmashauri.

Share To:

msumbanews

Post A Comment: