Wataalamu wa ardhi wa halmashauri ya Manispaa ya Ilemela wametakiwa kuzingatia sheria, taratibu, kanuni na miongozo ya utendaji wa kazi zao za kuhudumia wananchi ili  kuwaletea maendeleo wananchi wa Ilemela

Hayo yamesemwa na mkurugenzi wa utawala na rasilimali watu wizara ya ardhi nyumba na maendeleo ya makazi ndugu Zakaria Kera wakati wa kikao kazi kilichofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Halmashauri ya manispaa ya Ilemela ambapo amewaasa watumishi wa idara ya ardhi na vitengo vyake kuhakikisha wanatoa huduma bora kwa jamii kwa kuzingatia weledi na ufanisi uliotukuka kwani  ardhi ni mali ya umma.

“Ardhi ni mali ya wananchi, Na sisi ni watumishi wao ni wajibu wetu kuwahudumia kwa viwango vya ubora wa juu kabisa katika kujiepusha na migogoro  isiyokuwa ya lazima katika mambo mbalimbali yahusuyo ardhi.Wote tunatambua kasi ya serikali yetu ya sasa kufanya kazi kwa bidi na matokeo chanya hakukwepeki.”amesema ndugu Kera.


Aidha ndugu Kera amewataka watumishi hao kuheshimu maelekezo yanayotolewa na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela kwani wao sasa ni watumishi wa wizara ya ardhi moja kwa moja lakini kwa kuwa wanafanya shughuli zao ndani ya manispaa ya Ilemela ni budi kuendelea kushirikiana na ofisi ya Mkurugenzi pindi wanapohitajika kufanya hivyo .

Nae Mkurugenzi wa manispaa ya Ilemela ndugu John Wanga ameushukuru uongozi wa wizara ya ardhi kupitia ndugu Kera kwa mada mbalimbali za mafundisho juu ya uwajibikaji bora kwa watumishi wa ardhi.

“Najua mafundisho haya yatakuwa chachu katika utendaji wenu,kuepuka migogoro isiyo ya lazima ni jadi yetu toka tukiwa pamoja kwa karibu zaidi.Naamini wana Ilemela wanajivunia kazi yenu nzuri mnayoendelea nayo.Msilewe sifa lazima ubunifu katika kazi uendelee ili muendelee kuzaa matunda bora zaidi kwa manispaa yetu.”amesema ndugu Wanga.


Share To:

msumbanews

Post A Comment: