Waziri wa Katiba na Sheria Mhe Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba akisisitiza jambo wakati akizungumza kwenye kikao kazi na kamati ya ulinzi na usalama ya wilaya ya Kahama akiwa katika ziara ya kikazi ya siku moja Mkoani Shinyanga tarehe 15 Disemba 2020. 

(Picha Zote Na Mathias Canal, Wizara ya Katiba na Sheria)

Waziri wa Katiba na Sheria Mhe Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba akisisitiza jambo wakati alipotembelea shule Jerusalem English Medium mtaa wa Nyakato uliopo kata ya Nyasubi katika wilaya ya Kahama akiwa katika ziara ya kikazi ya siku moja Mkoani Shinyanga tarehe 15 Disemba 2020 kusikiliza na kutatua migogoro ya wananchi.

Waziri wa Katiba na Sheria Mhe Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba akisisitiza jambo wakati akizungumza kwenye kikao kazi na kamati ya ulinzi na usalama ya wilaya ya Kahama akiwa katika ziara ya kikazi ya siku moja Mkoani Shinyanga tarehe 15 Disemba 2020. 


Waziri wa Katiba na Sheria Mhe Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba akikagua shule yenye mgogoro ya Jerusalem English Medium mtaa wa Nyakato uliopo kata ya Nyasubi katika wilaya ya Kahama akiwa katika ziara ya kikazi ya siku moja Mkoani Shinyanga tarehe 15 Disemba 2020 kusikiliza na kutatua migogoro ya wananchi.

Waziri wa Katiba na Sheria Mhe Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba akizungumza na wananchi wanaoishi jirani na shule yenye mgogoro ya Jerusalem English Medium mtaa wa Nyakato uliopo kata ya Nyasubi katika wilaya ya Kahama akiwa katika ziara ya kikazi ya siku moja Mkoani Shinyanga tarehe 15 Disemba 2020 kusikiliza na kutatua migogoro ya wananchi.

Waziri wa Katiba na Sheria Mhe Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba akikagua Ramani ya shule yenye mgogoro ya Jerusalem English Medium mtaa wa Nyakato uliopo kata ya Nyasubi katika wilaya ya Kahama akiwa katika ziara ya kikazi ya siku moja Mkoani Shinyanga tarehe 15 Disemba 2020 kusikiliza na kutatua migogoro ya wananchi.

Na Mathias Canal, Wizara ya Katiba na Sheria-Shinyanga

Serikali ya awamu ya tano inayoongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Dkt. John Pombe Magufuli imejipambanua kuwalinda wanyonge hivyo anapojitokeza mtu yeyote kutaka kuwaumiza ni lazima ashughulikiwe kwa mujibu wa sheria na taratibu za nchi.

Waziri wa Katiba na Sheria Mhe Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba ametoa angalizo hilo tarehe 15 Disemba 2020 wakati akizungumza kwenye kikao kazi na kamati ya ulinzi na usalama ikiongozwa na Mkuu wa Wilaya ya Kahama Mhe Anamringi Macha akiwa katika ziara ya kikazi ya siku moja Mkoani Shinyanga.

Nchemba amekemea vikali wananchi wanaotaka kuijaribu serikali inayoongozwa na Mhe Rais Dkt Magufuli kwa kupora haki za watu hivyo ameeleza kuwa lazima watu hao waonyeshwe kwamba serikali haijaribiwi na haki za wananchi haziwezi kuchezewa.

"Msihangaike na jambo limetokea wapi badala yake uhalisia utumike kufanikisha utoaji wa maamuzi, ndugu zangu Rais wetu ana maono ya kutetea haki hivyo sisi  wasaidizi wake tunapaswa kuhakikisha kuwa wananchi wanatendewa haki pasina kuonewa" Alikaririwa Mhe Mwigulu Nchemba

Awali akisikiliza malalamiko ya mkazi wa Mtaa wa Nyakato Kata ya Nyasubi katika Halmashauri ya Mji wa Kahama Bi Specious Silvester anayemlalamikia aliyekuwa mume wake Ndg Richard Majenga kwa kumfanyia jaribio la kumuua kwa kummwagia Tindikali pamoja na kumzulumu mali zake, Mhe Mwigulu amesema kuwa Sheria na mahakama imechezewa vya kutosha hivyo ni lazima sasa jambo hilo lifike kikomo na hatua kali kuchukuliwa.

Katika kikao kazi hicho Waziri Nchemba amemuagiza Mkuu wa Wilaya ya Kahama Mkoani Shinyanga kuandaa na kusimamia utaratibu wa kisheria kuhakikisha kuwa hakuna jambo lolote litakalofanyika ikiwemo mauziano bubu ya mali za mlalamikaji huyo hadi pale shauri lililoko mahakamani litakapokamilika.

Pia ameagiza kuwa Wataalamu wa sheria katika Hamashauri ya Wilaya ya Kahama waandikishe kisheria kuzuia mpango ovu unaoendeshwa wa uuzaji mali huku kesi ipo mahakamani ambapo mpango huo ameutaja kuwa ni dharau kwa mahakama kadhalika ameagiza ufanyike uchunguzi wa haraka kuhusu mali zote za wawili hao.

Akizungumzia Mali zingine ambazo tayari zimeshauzwa na zingine zimesalia, Waziri huyo ameagiza zifuatiliwe zote na endapo itabainika umiliki wake ulikuwa wa watu wawili huku mmoja akiuza kinyume na utaratibu basi uchunguzi ukibaini mtu huyo akamatwe na kuchukuliwa hatua za kisheria haraka iwezekanavyo.

Kuhusu jaribio la kuua kwa mama huyo kumwagiwa tindikali, Mhe Dkt Mwigulu amesema kuwa halipaswi kuishia hewani lazima lipewe ukubwa namba moja na uchunguzi ufanyike upya ili sheria iweze kuchukua mkondo wake kwani jambo hilo limepelekea ulemavu wa kudumu kwa mama huyo.

Kadhalika Waziri Mwigulu ametoa angalizo kwa watendaji wote kutekeleza wajibu wao kwa wakati kwani amesema kuwa Sheria isipochukua mkondo wake  kwa wakati wananchi huchukua sheria mkononi katika kutafuta haki zao.

Kwa upande wake Silvester Model ambaye ni baba mzazi wa Specious Silvester ameipongeza serikali kupitia Waziri wa Katiba na Sheria kutembelea eneo lenye mgogoro pamoja na kufanya maamuzi ambayo yametoa taswira ya utendaji uliotukuka wa serikali ya awamu ya tano inayoongozwa na Mhe Rais Dkt. John Pombe Magufuli.

Share To:

Post A Comment: