Meneja Mradi wa kujenga Daraja kati sekta binafsi na sekta ya umma kutoka kampuni ya Trias Beatrice Minde akiongea na vyombo vya habari mapema leo jijini Arusha kwenye semina na wafanyabiashara wa viwanda picha zote na Ahmed Mahmoud Arusha  


Wafanyabiashara wakiwa kwenye picha ya pamoja mara baada ya semina hiyo ya siku moja lililoandaliwa kwa pamoja na Taasisi za Trias na Tccia na kufanyika jijini Arusha mapema leo picha zote na Ahmed Mahmoud Arusha 

Sehemu ya wafanyabiashara wakifuatili semina ya kutoa maoni na changamoto iliyoandaliwa kwa ushirikiano kati ya Taasisi za TCCIA na TRIAS kwa ufadhili wa shirika la maendeleo la umoja wa Ulaya iliyofanyika jijini Arusha zoezi hilo linafanyika katika mikoa 10 nchini.




 

 Na Ahmed Mahmoud Arusha 

Chama Cha wafanyabiashara wa viwanda mkoa wa Arusha TCCIA  kwa kushirikiana na shirika la Trias na Wizara ya Fedha kwa pamoja wamelenga kuwafikia wafanyabiashara wapatao 3000 kutambua changamoto wanazozipitia ili kuweza kushirikiana na serikali kuboresha sera na ufanyaji wa biashara nchini .

Akizungumza katika semina iliyowashirikisha wafanyabiashara wa jiji la Arusha Meneja wa mradi unaojulikana kwa jina la kujenga daraja Kati ya sekta binafsi na sekta ya umma Beatrice Minde alisema kuwa mradi huo ni sehemu ya ufadhili kutoka shirika la umoja wa Ulaya.

Alisema kuwa msingi mkubwa wa maoni hayo utasaidia serikali kupitia Wizara ya Fedha katika utungaji na uboreshaji wa sera na kuweka mazingira rafiki ya ufanyaji wa biashara nchini

Alisema mradi huo Ni wa miaka miwili umeanza mwezi January mwaka huu katika mikoa 10 lengo likiwa Ni kutambua changamoto za wafanyabiashara na baadae kuwasilisha serikalini kwa lengo la kutatuliwa na kufanyiwakazi na kuleta Tija katika kunyanyua sekta ya biashara nchini 

Kwa upande wake mratibu wa mradi huo Nebart Mwapwere alisema wao Kama daraja la kuwaunganisha wafanya biashara wameamua kufanya utafiti huo kwa kuwafikia wafanyabiashara kwa njia ya tehama au kieletroniki ambayo hukusanya maoni juu ya changamoto zinazowakabili. 

Alisema kuwa wamefikia mikoa 10 ikiwa ni Sera ya serikali ya awamu ya tano inayolenga kuboresha kutatua changamoto za wafanyabiashara wa kila Aina wakiwemo na wamiliki wa viwanda kutambua namna ya kufikisha mawazo yao kwa viongozi husika na kufanyiakazi ndio lengo la kufanya mijadala na wafanya biashara hapa nchini 

Alisema Kama wafanyabiashara wengi wa viwanda wamelalamikia kutozwa Kodi kubwa na kuwepo nanutitori ya malipo ya Kodi na kusema kuwa umeme nao ni sehemu ya matumizi makubwa ya uendeshaji wa viwanda na kutaka kupata punguzo 

Nae Slyvester Kazi Meneja Mauzo na Masoko ya Nje kutoka kampuni ya A to Z alisema kuwa Rais Dkt.John Magufuli anataka kuzalisha mabilionea wapya na semina hiyo ni mkakati wa serikali kuwakomboa wafanyabiashara wa kati na wa chini kufikia malengo ya kuwa mabilionea wapya.

Alisema kuwa wanaishukuru serikali kwa kuwashirikisha kutoa changamoto zao nini kifanyike hii inaonyesha dhamira ya dhati ya serikali kufikia malengo na maono ya mh.rais wetu ikiwa ni utekelezaji wa sera ya uchumi wa kati wa viwanda

Share To:

Arusha Newsroom

Post A Comment: