NA NAMNYAK KIVUYO, ARUSHA.


Mbunge wa Arusha mjini Mrisho Gambo kwakushirikiana na wadau wa maendeleo wamewagawia viti mwendo walemavu 100 kati ya 565 wa jiji la Arusha ili kuondoka changamoto ya usafiri.


Akizungumza wakati wa zoezi hilo lililofanyika katika ofisi ya mkuu wa wilaya ya Arusha mjini,Gambo alisema utaratibu huo ni endelevu kwani waliobaki zoezi lingine la utoaji litakuwa Januari 2021 na litakuwa sambamba na ugawaji wa kadi za bima ya afya.


"Tunafanya haya kwasababu tunaamini kwamba kundi hili ni muhimu na ni sawa na binadamu wengine na sisi kama viongozi tunatakiwa tushirikiane katika kuwatengenezea mazingira wezeshi walemavu ili waweze kupata vifaa vya kuwasaidia kupambana na maisha kama watu wengine,"alisema Gambo.


Alisema wapo walemavu ambao wanahitaji maeneo ya kufanyia biashara hivyo atazungumza na wenye maeneo mbalimbali ili kuwasaidia na kuwawezesha wapate kipato cha kuwasaidia kwani sisi kama viongozi kazi yetu ni kuwatafutia fursa.


Alieleza kuwa anafahamu kuwa katika halmashauri, walemavu wanafungu la asilimia 2 hivyo atashirikiana na madiwani ili kuhakikisha utaratibu maalumu wa kuwapatia mafunzo ya upataji elimu ya ufanyaji biashara  na kuwza  kutumia mikopo ya halmashauri na kurejesha kwa wakati.


Kwa upande wake mtaalam na mratibu wa viti mwendo wa CCBRT, Neophita Athanas alisema viti hivyo ni moja ya matibabu ya kuweka mwili sawa hivyoni vyema wakavitunza ikiwa vifaa hivyo ni vya gharama kwani kiti kimoja hugharimu sh.laki 3 hadi 7 kwani vimetofautiana matengenezo kutokana na aina ya ulemavu wa mtu aliyonao.


"Viti hivi mkiviacha ovyo vinaweza kuibiwa  kwa ajili ya vyuma chakavu kwani asili yake kubwa ni chuma hivyo mkifanya hivyo mkivitunza mtakuwa mmemshuku mbunge wenu lakini ikiwa kinyume mtakuwa mmemuangusha  lengo lake kwani amejitoa hata sehemu yake ya familia ili kusaidia kuondokana na chngamoto,"alisema.


 Mwenyekiti wa walemavu jiji la Arusha,Martha Edimund alisema anamshukuru Mbunge kwa kushirikiana na wadau hao katika kufanikisha zoezi hilo kwani walilisubiri muda mrefu bila kutokea kwa viti mwendo ambavyo ni tiba kwa walemavu hivyo huduma hiyo ni ya kipekee kwao.


"Nawaasa walemavu wenzangu pamoja na walezi na wanaojisimamia wenyewe kutumia vifaa hivyo kikamilifu kwa kuzingatia maelekezo waliopewa na wataalamu kwasababu vifaa hivyo ni vya kudumu na vinatuongezea hatua yenye mafanikio pamoja na ufanisi ,"alisema.

Share To:

msumbanews

Post A Comment: