NA NAMNYAK KIVUYO, ARUSHA.


Diwani wa Kata ya Sekei jimbo la Arusha mjini Gerald John Sebastian amekabidhi mpira kwa timu ya mpira wa miguu ya kata hiyo ikiwa ni sehemu ya kutekeleza ahadi zake alizozitoa katika kampeni za uchaguzi mwaka huu.


Akikabidhi Mpira huo Sebastian alisema kuwa ateandelea kutekeleza yale yote aliyoahidi wakati akijinadi  huku akihakikisha ilani ya chama cha mapinduzi (CCM) inatekelezwa katika katika kata yake ili kuwaletea wananchi maendeleo na kutatua kero zinazowakabili.


Alisema kuwa wananchi  wa kata yake wamefanya kazi kubwa ya kuipa CCM ushindi kwanzia diwani, mbunge na Rais hivyo kwa kushirikiana na viongozi wenzake watarudisha shukrani kwa kutekeleza yote waliyoahidi katika majukwaa ya kampeni ikiwa ni pamoja na kusimamia na kuhakikisha yote aliyoahidi Rais John Magufuli kwa wananchi  yanatekelezeka.



Alieleza kuwa aliahidi kununua mpira kwaajili ya timu ya kata na sasa ametekeleza kakini pia aliahidi wananchi  endapo watamchagua Rais John Pombe Maghufuli  kuwa Rais wa nchi kwa mara nyingine, Mrisho Gambo kuwa Mbuge jimbo la Arusha mjini nayeye kuwa diwani wa kata hiyo atawatumikia masaa 24 bila kuchoka na yupo tayari kufanya hivyo.


“Niliahidi kutuwatumikia wananchi wakiwapa CCM ushindi katika ngazi zote na wamefanya hivyo  na sasa nimeshaanza kuwatumikia, muda wowote nipo tayari hivyo wananchi msisite kuleta changamoto kwangu kama nilivyowaahidi nitatekeleza,” Alisema Sebastian.


“Nitahakikisha changamoto zote zinazowakabili wananchi wa Sekei zinapata ufumbuzi, ambazo naweza kuzitatua peke yangu nitazitatua na zile ambazo zinahitaji nguvu ya serikali kwa maana ya maamuzi kutoka baraza la madiwani halmashauri na ngazi zingine nitaziwasilisha na kwa kushirikiana na halmashauri yetu ya jiji la Arusha, wilaya na mkoa kwa ujumla majawabu yote yatapatikana,”Alifafanua



Alieleza kuwa aliahidi kutatua changamoto nyingi zilizokosa ufumbuzi kwa muda mrefu katika kata hiyo ikiwemo, ujenzi wa shule ya sekondari ya kata ambayo kwa sasa wapo katika mchakato wa kuangalia ni jinsi gani wanalitafututia ufumbuzi na katika hili atahakikisha anashirikiana kikamilifu na wananchi ili shule ya kata iweze kupatikana.


 “Sasa nataka kukidhi  kiu ya wana Sekei kwa kujenga shule ya sekondari  ya Kata ya Sekei hii ndio ndoto yangu kubwa, niliwaambia mkinichagua mtakuwa mmelamba dume, maendeleo yote mnayotakiwa kuyapata mtayapa na kata hii ina ofisi karibia zote za  serikali nitashirikiana na nyie wananchi na viongozi wa serikali kuhakikisha  maendeleo yanapatikana kwa haraka,” Alisema.



Kwa upande wao baadhi wachezaji wa timu hiyo Jackson Richard alisema kuwa diwani huyo amewafanyia jambo ambalo walikuwa na uhitaji nalo kakini pia amewaahidi kuanzisha ligi, kuwanunulia jezi na kuendelea kutatua changamoto ya mpira kila watakapohitaji na kwa kuwa wanawaamini viongozi wanaotokana na Chama cha mapinduzi wanajua atatekeleza kikubwa ni kumpa muda.


Naye Hatibu Abdi alieleza kuwa wanataka viongozi ambao wanaona changamoto za vijana na kuzitatua kwani kwa msaada wa mpira huo alioutoa diwani huyo itawasaidia kuwaweka vijana pamoja na kushirikiana katika mambo mbalimbali yakiwemo ya kijamii.


Aidha mwenyekiti wa tawi la CCM kata Sekei Richard Temba alisema kuwa ndani ya mwezi mmoja na nusu wameshaanza kutekeleza waliyoyaahidi ambapo pia diwani aliahidi kuvuta umeme katika soko la Sanawari na jambo hilo limeshafanyika sasa hivi soko lina umeme wananchi wanafanya shughuli zao kwa furaha kwani changamoto ya kukosa huduma ya umeme ilikuwa kero kubwa kwao.


“Na sio haya tuu utekelezaji unaendelea hivyo niwaombe wananchi kuendelea kuwa na imani na CCM kwani wana viongozi makini wanaojali maendeleo ya wananchi,” Alisema Temba.

Share To:

msumbanews

Post A Comment: