NA HERI SHAABAN


SHULE ya Sekondari  Juhudi Halmashauri ya Ilala wajivunia mafanikio yake kitaaluma  kwa kufanya vizuri kila mwaka. 

Hayo yalisemwa katika mahafali ya 13 ya kidato cha nne na Mkuu wa Shule ya Juhudi Dellvine Koka wakati wa kutoa vyeti kwa wahitimu. 

Dellvine alisema  shule ya Sekondari ya Juhudi ilianzishwa 2002 ilizinduliwa na aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salam Yusuph Makamba ikiwa na vyumba vinne na wanafunzi 45.

 Akielezea mafanikio ya kitaaluma alisema matokeo ya kidato cha pili 2013 mpaka 2016 shule hiyo imekuwa ikifanya vizuri ambapo  mwaka 2013 imefaulisha  kwa asiimia 95.75,Mwaka 2014 imefaulisha kwa asilimia 98.2,Mwaka 2017asilimia 94.1 mwaka asilimia 96.1 mwaka 2019 asiimia 96.8 na 2020 imefaulisha kwa asilimia 98.9.

Akielezea ufaulu wa kidato cha nne mwaka 2018  Wanafunzi 388 walifanya mtihani wanafunzi 121 walichaguliwa kidato cha tano mwaka 2019 jumla ya wanafunzi 409 walifanya mtihani wanafunzi 132  walichaguliwa  kidato cha tano mwaka 2020 Jumla ya wanafunzi 362 walifanya mtihani jumla ya Wanafunzi 176 walichaguliwa kidato cha tano

"Mafanikio ni mazuri katika shule yetu ya sekondari Juhudi  Kitaaluma tupo vizuri  kwa sasa shule ina Walimu 92 wa kike 60 wa kiume 32  akielezea idadi ya Wanafunzi  wa kidato cha kwanza hadi kidato cha nne, 2003 Wavulana 1002 na Wasichana 1001  na wanafunzi wa kidato cha tano 384 kati yao Wasichana 177  Wavulana 207 " alisema Dellvine


Dellvine alisema kutokana shule hiyo kufanya vizuri kitaaluma na kuwa na kipaji katika sekta ya michezo imepandishwa hadhi na kupandishwa kidato cha tano Julai 2016 michepuo iliyoanzishwa shuleni hapo HGL, HGE na HGK


Aliwataka wanafunzi wa shule hiyo kuzingatia masomo kila wakati pamoja na nidhamu wawapo shule na nyumbani 


Kwa upande wake Mgeni rasmi Mbunge wa Afrika Mashariki Dkt. Ngwaru Magembe aliwataka wasome kwa bidii na kumtanguliza Mwenyezi Mungu kila Wakati. 


Katika Mahafali hayo Dkt Magembe alichangia shilingi milioni harambe ya shule hiyo kwa ajili ya kutunisha mfuko. 

Share To:

msumbanews

Post A Comment: