Na John Walter-Babati

Taasisi ya Kuzuia na kupambana na rushwa mkoa wa Manyara , imemfikisha mahakamani Mtumishi wa baraza la ardhi wilaya ya Babati,  Ruth Reniel Semkuyu kwa makosa ya kudai na kuomba rushwa ya shilingi laki moja.

Akisomewa mashtaka  hayo mbele ya hakimu  Mkazi wa mahakama ya mkoa wa Manyara, Mwendesha Mashtaka wa Takukuru Evelyne Onditi ameeleza kuwa,  kesi ya Jinai namba CC.155/2020 imesomwa Septemba 9 mwaka huu mbele ya Mheshimiwa Hakimu mkazi mfawidhi wa Mahakama hiyo  Mheshimiwa Simon Kobelo.

Mwendesha mashtaka huyo amesema, baada ya kusomewa Mashtaka hayo, mtuhumiwa huyo alikana na kurudishwa rumande baada ya kushindwa kutimiza masharti ya dhamana.

Onditi amesema kesi hiyo itatajwa tena Mahakamani hapo Septemba 23,2020.
 
Share To:

Post A Comment: