Mgombea Urais wa CHAUMA,Hashim Rungwe

Chama cha Ukombozi wa Umma( CHAUMA) kimezindua rasmi kampeni zake leo na kuahidi kuhakikisha wanashughulikia mpango wa watoto kupata chakula mara tu watapoingia madarakani.

Hayo yamesemwa leo Septemba 5 Jijini Dar es Salaam na mgombea wa nafasi ya Urais wa chama hicho, Hashim Rungwe alipokuwa akinadi sera zake na kusema siku ishirini za mwanzo ni za mpango wa watoto kupata chakula.

"Mimi nikiingia pale nawahakikishieni kitu cha kwanza watoto wapate chakula, siku ishirini za kwanza ni mipango ya watoto shule", amesema Hashim Rungwe.

Aidha Rungwe amesema kuwa chama chake kikingia madarakani kitaendesha serikali kwa kuzingati haki na kwamba viongozi wakubwa hawatatumia magari ya gharama kubwa.

"Watumishi wote wa Serikali hakuna aliyeongezwa mshahara miaka 5 inawezekana kweli?. Wale wanaopita barabarani wote si wameshiba, mimi nawaambia siku za kwanza magari nitayauza DC atapanda Land Rover Defender",amesema Rugwe.

Chanzo - EATV
Share To:

msumbanews

Post A Comment: