.
Mkuu wa wilaya ya Monduli Mheshimiwa Iddi Kimanta amewapongeza walimu kwa kuwatendea haki wananchi Monduli kuchapa kazi na kuongeza ufaulu katika mitihani kitaifa.


Ameyasema hayo katika semina iliyoandaliwa na Idara ya Elimu Msingi kwa lengo la kuwakutanisha walimu wakuu wote wa shule za msingi na shule za binafsi zilizo ndani wilaya ya monduli ili kutathmini na kuweka mikakati ili kujiandaa kabla shule kufunguliwa .

Mkuu wilaya amewataka walimu kuenda kufanya kazi na kuhakikisha Wilaya haishuki kitaaluma,Wilaya Kupitia idara ya Elimu msingi chini Theresia kyara  imendelea kufanya vizuri mfululizo kwa ukuaji elimu Mwaka  2017 Ukujaji umekuwa kwa asilimia 69.8.6,Mwaka 2018 ukuaji asilimia 85.1.6 na 2019 ukuaji asilimia 92.0.1 huku Monduli imendelea kufanya vizuri katika mitihani ya Kitaifa 2018-Nafasi 45
2019-Nafasi 25 hivyo amewataka walimu wakirudi shuleni wasitumie ugonjwa Covid_19 kama kisingizio   kushusha taaluma bali wafanye kama fursa kwao kwa kufanya vizuri zaidi na kuongeza ufaulu.


Mkuu wa idara ya Elimu  Msingi Theresia Kyara, amewataka wazazi kuleta wanafunzi shuleni kwa wakati kwani shule zikifunguliwa tuu vipindi vitaanza na anapenda kuwaondolea hofu wazazi kuwa wanafunzi ktk shule za kutwa na bweni watakuwa salama kwani  Halmashauri na idara ya Elimu msingi imeshajipanga kikamilifu katika kuwawekea mazingira salama wanafunzi kujisomea na tahadhari zote za kujilinda na Ugonjwa wa covid 19 zimechukuliwa.

DC KIMANTA APONGEZA WALIMU.

DC KIMANTA
DC MONDULI

Imetolewa na Ofisi ya mkuu wa Wilaya ya Monduli.🇹🇿
IJUMAA
19/06/2020.
ELIFURAHA RAPHAEL(KABURU).
Share To:

Post A Comment: