Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi,Vijana Na Ajira Mh Anthony Mavunde ametoa rai kwa Watanzania kuunga mkono bidhaa zinazozalishwa na Vijana wa Tanzania kwa kuwa soko  la bidhaa zao.

Naibu Waziri Mavunde ameyasema hayo leo Jijini Mwanza alipotembelea Kiwanda cha Vijana cha Soma bags cha mabegi ya wanafunzi ambacho kimepewa mkopo wa Tsh 30,000,000 kupitia Mfuko wa maendeleo ya Vijana-YYD

"Mkopo mlioupata mmeutumia vyema na kuongeza uzalishaji kwa kiwango kikubwa,ninyi mnatuma ujumbe muhimu sana kwa vijana wengi nchini kwamba Vijana wanaweza kufikia mafanikio kupitia mifuko hii ya uwezeshwaji ya Serikali.

Nitoe rai kwa Watanzania wote kuunga mkono bidhaa zinazozalishwa na Watanzania hasa vijana,Shule zote za
msingi na Sekondari hapa Mwanza na mikoa ya Jirani mnaweza kuwa soko la ukakika wa mabegi yanayozalishwa hapa Kiwandani"Alisema Mavunde

Akitoa maelezo ya awali,muasisi wa Kiwanda cha Soma bags Ndg Innocent James,ameishukuru sana Serikali ya awamu ya Tano chini ya Mh Rais Dr.John Pombe Magufuli kwa namna ambavyo imewawezesha na kupanua shughuli za uzalishaji kutoka mabegi 20 kwa siku mpaka mabegi 100 na kuongeza Ajira mpaka kufikia Vijana 21 kutoka Vijana 8 wa awali.

Katika kuunga mkono jitihada za shughuli ya Kampuni hii ya Vijana,Halmashauri ya Jiji la Mwanza wameahidi kushughulikia na kuwapatia mkopo Vijana hawa  wa Tsh 60,000,000 kwa ajili upanuzi wa shughuli za Kiwanda.
Share To:

Post A Comment: