Klabu ya Azam FC inatarajia kucheza mchezo wa pili wa kirafiki dhidi ya KMC, utakaofanyika Uwanja wa Azam Complex siku ya Jumatano saa 1.00 usiku.

Mchezo huo utakuwa wa mwisho wa kikosi hicho, kabla hakijacheza na Mbao, kwenye mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara (VPL) utakaofanyika dimbani hapo Juni 14, saa 1.00 usiku.

Benchi la ufundi la Azam FC chini ya Kocha Mkuu, Aristica Cioaba, litautumia mchezo huo kukiangalia kiufundi kwa mara ya mwisho kabla ya kuanza tena kwa patashika ya ligi.

Ikumbukwe kuwa siku ya Jumamosi, kikosi cha Azam FC kilicheza mchezo wa kwanza wa kirafiki dhidi ya Transit Camp, ulioisha kwa suluhu.
Share To:

Post A Comment: