SALVATORY NTANDU
Jeshi la Polisi mkoani Shinyanga linawashikilia  watu  48 kwa tuhuma za kufanya makosa mbalimbali katika jamii ikiwemo uhalifu pamoja na kukutwa na mali zinazodhaniwa ni za wizi.

Akizungumza na Waandishi wa habari jana, Kamanda wa Polisi mkoani humo,ACP Debora Magiligimba amesema watuhumiwa hao walikamatwa baada ya jeshi hilo kufanya msako maalum kwa kipindi cha miezi mine mfululuzo na kufanikiwa kukamata mali hizo.

Amesema kuwa msako huo ulianza mwezi  Disemba mwaka Jana hadi Machi, mwaka huu katika maeneo mbalimbali ya wilaya ya  Shinyanga na kufanikiwa kuwanasa watuhumiwa hao, ambapo 28 wamelishafikishwa mahakamani huku 20 mashauri yao yanaendelea kuchunguzwa.

Kamanda  Magiligimba amevitaja vitu  vilivyokamatwa katika msako huo ni pamoja na  pamoja na pikipiki, runinga,Tarakalishi, vitenge, mchele, mapipa kutengenezea pombe haramu aina ya Gongo, magodoro Baiskeli, na dawa za kulevya mirungi na bangi.

Katika hatua nyingine kamanda  Magiligimba  ametaka wananchi kuwa makini katika kipindi hiki cha kuelekea sikukuu ya Pasaka  kwa kusherehekea kwa amani bila kwenda  kwenye kumbi za starehe na kuwataka kujiepusha na mikusanyikao isiyokuwa na tija.
Share To:

msumbanews

Post A Comment: