
Kaimu
Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi (Sekta ya Uvuvi), Magese
Bulayi,akizungumza wakati akifungua Warsha ya Kuwajengea Uelewa
Watalaamu wa Uvuvi kuhusu Mwongozo wa Hiari wa kuhakikisha Uvuvi Mdogo
unakuwa endelevu nchini iliyofanyika jijini Dodoma.



Sehemu
ya washiriki wakifatilia hotuba ya Kaimu Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo
na Uvuvi (Sekta ya Uvuvi), Magese Bulayi, wakati akifungua Warsha ya
Kuwajengea Uelewa Watalaamu wa Uvuvi kuhusu Mwongozo wa Hiari wa
kuhakikisha Uvuvi Mdogo unakuwa endelevu nchini iliyofanyika jijini
Dodoma.


Kaimu
Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi (Sekta ya Uvuvi), Magese
Bulayi,akiwa katika picha ya pamoja na washiriki mara baada ya kufungua
Warsha ya Kuwajengea Uelewa Watalaamu wa Uvuvi kuhusu Mwongozo wa Hiari
wa kuhakikisha Uvuvi Mdogo unakuwa endelevu nchini iliyofanyika jijini
Dodoma.
......................................................................................................................
Na.Alex Sonna,Dodoma
Kaimu
Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi (Sekta ya Uvuvi), Magese
Bulayi,amesema kuwa asilimia 95 ya mapato yanayopatikana kwenye Uvuvi wa
mazao ya Samaki katika bahari,maziwa,mabwawa na mito kwa mwaka
huchangiwa na wavuvi wadodo nchini.
Hayo
ameyasema leo jijini Dodoma wakati akifungua Warsha ya Kuwajengea
Uelewa Watalaamu wa Uvuvi kuhusu Mwongozo wa Hiari wa kuhakikisha Uvuvi
Mdogo unakuwa endelevu nchini.
Bw.Bulayi
amewataka watalaamu hao kutoa maoni yao kwa uhuru yatakayosaidia
kuandaa Mpango wa Utekelezaji wa Mwongozo wa hiari kuhakikisha uvuvi
mdogo unakuwa endelevu nchini.
Hata
hivyo amesema kuwa sekta ya uvuvi kote duniani kama vile nchini ni
muhimu sana, kulingana na takwimu za Shirika la Chakula na Kilimo la
Umoja wa Mataifa (FAO) watu milioni 120 duniani wanajishughulisha na
shughuli za uvuvi.
“Kati ya asilimia 90 wameajiriwa au kujiajiri katika uvuvi mdogo, ambapo kati ya hao, asilimia 50 ni akinamama,” alisema.
Aidha
Bulayi amesema kuwa asilimia 90 ya watu waliopo katika uvuvi mdogo wamo
katika nchi zinazoendelea na hivyo kiwezesha asilimia 95 ya samaki
wanaovuliwa na wavuvi wadogo kitumiwa katika nchi zinazoendelea na hatua
hii itasaidia sana kuhakikisha usalama wa chakula katika nchi zetu.
Bulayi
amesema kuwa katika hali ya kushangaza katika kundi hilo la wavuvi
wadogo watu milioni 5.8 wanaishi kwa kipato cha chini ya wastani wa dola
moja ya kimarekani kwa siku ambayo ni sawa na sh 2,200 za kitanzania.
Amesema
kuwa si jambo jema kujisifia kwamba tuna rasmali nyingi za uvuvi na
zenye thamani kubwa, wakati watu wanaoshiriki shughuli za uvuvi wamo
katika lindi la umasikini mkubwa.
Hata
hivyo amesema amesema kuwa Serikali imekuwa ikijitahidi sana kutatua
changamoto wanazokumbana nazo wavuvi ikiwa ni pamoja na ukosefu wa
mitaji na mikopo, matumizi ya teknolojia duni, upotevu wa mazao
yaliyovunwa na ugumu wa kuyafikia masoko.
"Hatua
zilizochukuliwa na Serikali katika kusaidia kutatua changamoto hizo ni
pamoja na kuandaa Sera ya uvuvi, sheria, kanuni na miongozo mbalimbali
ya mpango kabambe wa kuendeleza sekta ya Uvuvi."
Naye
mwenyekiti wa kikosi kazi cha Taifa cha kutekeleza mwongozo wa hiari wa
kuendeleza uvuvi mdogo, Bw. Yahya Mgawe amesema kuwa Serikali imeweka
mfumo wa huduma za ugani ambazo zinatolewa katika Halmashauri karibu
zote nchini, hii ni pamoja na huduma za utoaji mafunzo ya uvuvi na
ufugaji samaki ambayo yanatolewa sehemu mbalimbali nchini.
"Pamoja
na juhudi zetu zote hizi, hali ya wavuvi wadogo bado haijafikia
matamanio ya Serikali, kipato chao, vyombo wanavyotumia, mitego
wanayotumia ni duni na hawawezi kwenda kwenye maeneo ambayo yana samaki
wengi." Amesema Mgawe.
Kwa
upande wake Mwakilishi wa FAO, Dk Oliver Mkumbo ameishukuru Serikali
kwa kuandaa warsha hii ya kujenga uelewa na kukusanya maoni
yatakayosaidia kuandaa mpango wa utekelezaji wa mwongozo wa hiari wa
kuhakikisha Uvuvi mdogo unakuwa endelevu Tanzania kwani itasaidia wavuvi
kutoka kwenye dimbwi la umaskini na kujiongezea kipato kutokana na
uvuvi.
Post A Comment: