NA HERI SHAABAN
MKUU wa Wilaya ya Ilala Sophia Mjema amewataka wananchi wa Wilaya ya Ilala ifikapo Novemba 24 kuchagua viongozi wa Serikali za Mitaa wenye sifa.
Mjema aliyasema hayo katika ziara yake kata ya Jangwani ,Upanga Mashariki na Upanga Mangharibi.
“Novemba 24 mwaka huu tunatarajia kushiriki katika chaguzi za Serikaĺi za Mtaa kuchagua Wenyeviti wa Serikali za mtaa watakaokuja kuongoza wananchi rai yangu wanachi chagueni wenyeviti wenye sifa waje kutatua kero zenu pamoja na kuisaidia Serikali”alisema Mjema
Mjema aliwaka wanachi kutumia fursa hiyo ya kupiga kura kila mmoja kutumia haki yake kwani ni sehemu Demokrasia.
Alisema serikali ya awamu ya tano ya Rais John Magufuli kauli mbiu yake Tanzania ya uchumi wa viwanda nchi yetu imefanikiwa kuongeza viwanda na miradi mikubwa ya kisasa ametaka wananchi kuchagua viongozi wa mtaa wenye sifa watakao leta chachu ya maendeleo.
Kwa upande wake Afisa Ustawi wa Jamii Ilala Joyce Maketa alielezea opalesheni endelevu ya kuwakamata ombaomba alisema opalesheni inafanyika usiku wanawakamata watoto na wakubwa.
Maketa alisema katika opalesheni hiyo wanawakamata katika makundi mawili watoto na wakubwa watoto wanaifadhiwa halmashauri wanapelekwa shule na wakubwa wanapelekwa mahakama ya JiJi.
Maketa alitoa wito kwa wana Ilala waache tabia ya kusaidia ombaomba badala yake misaada yote ipelekwe kwa ofisa Ustawi wa Jamii ili wagawe katika vituo vya yatima.
Post A Comment: