Na.Faustine Gimu Galafoni,Dodoma.
Chama cha Wabunge wanawake walio chini ya Jumuiya ya madola kwa kanda
ya Afrika kinatarajia kuanza semina itakayowalenga wanachama wa chama
hicho.

Akizungumza na Waandishi wa Habari bungeni jijini Dodoma,Spika wa bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Job Ndugai amesema Semina hiyo itafanyika kuanzia tarehe,26-29/10/2019
jijini Arusha itakayohusu masuala mbalimbali ya Wanawake ikiwa ni
pamoja na Uchaguzi.

Mhe,Ndugai ametaja washiriki mbalimbali katika Semina hiyo ni asasi za
kiraia na serikali zinazohusu masuala ya Wanawake huku nchini
zilizokubali ushiriki wa semina hiyo hadi sasa  ni pamoja na
Afrikakusini,Botswana,Eswatin[Swaziland]Ghana,Cameroon,Lesotho,Malawi,Kenya,
Nigeria,Namibia,Rwanda,Msumbiji , Mauritania ,SierraLeone,Tanzania,Uganda na Zambia.

Aidha,Mhe,Ndugai amesema hadi Sasa Tanzania kila halmashauri ina
madiwani wanawake chini ya  asilimia 30%,bungeni ni asilimia 36.6% ya
wabunge wote  ni wanawake na Mawaziri ni 11 kati ya 45 ni wanawake
huku Majaji ni 19 katika 88 ni wanawake na nchi ya Rwanda ikitajwa
kuwa  nchi ya Wabunge wanawake wengi zaidi kuliko wanaume.

Wanachama wa Mabunge ya Jumuiya ya Madola ukanda wa Afrika kuna jumla
ya Mabunge 46 ambapo Afrika kusini  Mabunge 9,Nigeria Mabunge 36 na
Tanzania ni Bunge 1 ambalo ni la baraza la Wawakilishi,  Zanzibar.

Sanjari na hayo,Mhe.Ndugai amesema baada ya bunge la Mwezi Novemba
,2019 kuisha yatabaki mabunge mawili tu kabla ya kuingia uchaguzi mkuu
,2020 ambapo Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania,atalifunga Rasmi
Mwishoni mwa Mwezi Juni,2020 .
Share To:

msumbanews

Post A Comment: