Marais
Yoweri Museveni wa Uganda na Paul Kagame wa Rwanda wamesaini
makubaliano ya amani katika mji mkuu wa Angola, Luanda, kumaliza uhasama
uliopo kati ya mataifa hayo jirani.
Walifikia
makubaliano hayo katika mkutano huo wa pili mbele ya marais wa Jamhuri
ya Kidemokrasia ya Congo, Angola na Congo Brazzaville waliokuwa
wapatanishi katika mgogoro huo.
Joto
la kisiasa limekuwepo tangu mwanzoni mwa mwaka huu na limeathiri maisha
ya watu kijamii na kiuchumi katika mataifa hayo jirani.
Maofisa
nchini Rwanda wameishutumu Uganda kwa kuwafunga na kuwatesa kinyume cha
sheria raia wake nchini Uganda, wakati Uganda nayo inaishutumu Rwanda
kutekeleza ujasusi katika ardhi yake.
Post A Comment: