Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazinigira), George Simbachawene ametaka kuwepo utunzaji wa ekolojia katika Maporomoko ya bonde la kihansi kwa faida ya nchi kwa kizazi cha sasa na baadaye kutokana na umuhimu wake kimazingira.
Ameyasema hayo katika ziara yake ya bonde la maporomoko ya mto kihansi yaliyopo wilayani kilombero mkoa wa Morogoro na kufanya zoezi la kurejeleza vyura wa kihansi katika maeneo yao ya asili kama sehemu ya ziara yake.
Amesema Ekolojia iliyopo katika bonde hili ni muhimu kutunzwa kutokana na upekee wake hali itakayoleta faida kwa vizazi vya sasa na vya baadaye.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa Baraza la Taifa la Usimamizi wa Mazingira (NEMC), Dkt.Samuel Gwamaka amesema Baraza lake litaendelea kufanya usimamizi na uhifadhi katika eneo hilo kwa kushirikiana na wadau wengine wa mazingira.
Waziri Simbachawene amekuwa ni Waziri wa pili kupanda maporomoko ya Bonde la mto Kihansi na kufanya zoezi la kurejeleza vyura wa kipekee dunia, Waziri wa kwanza kupanda katika bonde hili alikuwa Prof.Mark Mwandosya
mwaka 2006.
Post A Comment: