Ndege yaanguka na kuteketea kwa moto kando ya uwanja wa Ndege wa Mafia muda mfupi baada ya kuanza safari yake kuelekea Dar es Salaam.

Taarifa za awali zinaeleza kuwa ndege hiyo ilianza safari yake kutoka katika uwanja wa ndege wa Mafia ikiwa na abiria 8 watano kati yao wamepatikana wakiwa ni majeruhi ambao wanapatiwa matibabu katika hospitali ya Wilaya ya Kilinodoni ( Mafia) huku wengine watatu taarifa zao zikiwa bado hazijafahamika.

Mamlaka za usalama bado zinaendelea na zoezi la uokoaji na zimeeleza kuwa zitatoa taarifa zaidi zoezi litakapokamilika.
Share To:

msumbanews

Post A Comment: