Naibu waziri wa Maji Mhe. Juma  Aweso, ameagiza jeshi la Polisi Wilaya ya Arumeru kuwashikilia na kuwaweka chini ya ulinzi  viongozi wanne wa  bodi ya  Maji MAKILENGA  Halmashauri ya Meru,Wilayani Arumeru kwa kutuhumiwa  za kufanya ubadhirifu kwenye Mradi huo.
Aweso ametoa agizo hilo baada ya kubaini uwepo wa ubadhirifu wa fedha za mradi huo licha ya makusanyo  ya fedha zinazotokana na uchangiaji wa huduma ya maji kufika  kiasi cha milioni tano (5) kila mwezi bodi imebakiwa na kiasi kisichozidi milioni moja na nusu tu,  “Haiwezekani asilimia kubwa ya mradi unatumia vyanzo vya mtiririko matum izi yake kuwa makubwa kiasi cha kumaliza fedha zote za miaka minne”amehoji Aweso.
Waliokamatwa kwa tuhuma za kuhujumu mradi huo ni pamoja na mwenyekiti wa Bodi Godhope Chales,Mhasibu wa Mradi Bi.Warialanga Pallangyo,pamoja na fundi bomba wa mradi huyo anayetambulika kwa jina la Kaaya.Meneja wa Mradi huo Orest Manyanga amewekwa chini ya ulinzi kwa kuonesha utovu wa nidhamu wakati wa kikao cha Naibu waziri na wajumbe wa bodi ya MAKILENGA.
Aidha Aweso ameridhishwa na utekelezaji wa Mradi wa Maji Kiiji cha Kingori wenye thamani  ya Shilingi bilion 1.5 sambamba na kumpongeza mkandarasi kwa utendaji mzuri chini ya usamizi wa Uongozi wa Wilaya hiyo.
Haya yamejiri wakati wa ziara ya Naibu huyo Wilayani Arumeru iliyolenga kutembelea na kukagua Miradi ya Maji ili kuweza kutambua na kuzitafutia ufumbuzi changamoto zinazokwamisha utekelezaji wa Miradi ya maji kwa kuzingatia utekelezaji wa Ilani ya uchaguzi ya Chama cha Mapinduzi imeelekeza mpaka kufikia 2025 upatikanaji wa maji vijijini kuwa asilimia 85 na mjini 95,
Mkuu wa Wilaya ya Arumeru akieleza namna Wilaya hiyo inavyosimamia utekelezaji wa Miradi ili wananchi waweze kunufaika. 
Mhe.Mbune wa Jimbo la Arumeru Mashariki John Pallangyo akiishukuru Serikali kusikia kilio alichowasilisha Bungeni  cha wananchi Wameru kuhusu maswala ya Maji kilichopelekea Naibu waziri wa Maji kufanya ziara Wilayani hapo ili kutatua changamoto hiyo.
Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri ya Meru,Nelson Mafie ameipongeza Serikali kwa utatuzi wa changamoto za wananchi  ambapo imeunda chombo cha wakala wa maji vijijini na Mjini (RUWASA)."huu ndio Mwarubaini wa changamoto za ya maji "amesisitiza Mafie.
Wananchi wamempongeza Mkuu wa Wilaya ya Arumeru Jerry Muro  kwa kutumia fedha zake kumgaramia nauli ya Mzee Senyaeli Mbise Maarufu kama  Lemali, ambaye ni fundi mwenye uelewa wa mradi wa Maji MAKILENGA kurudi kuendelea na kazi hiyo baada ya fundi aliyekuwepo kuwa kikwazo kwenye utendaji.
wsjumbe wabodi ya MAKILENGA,viongozi na wanachi na wataalamu wakifuatilia kikao
viongozi na wanachi na wataalamu wakifuatilia kikao
Viongozi na wananchi wa Kata ya Kingori wakifuatilia kikao.
Share To:

msumbanews

Post A Comment: