Mkuu wa Wilaya ya Magu, Dkt. Philemon Sengati ( PhD) ametoa onyo kali huku akiwaagiza watendaji katika halmashauri hiyo kuwamata watu wanaokata miti hovyo bila kupanda hususan miti ya matunda kwa lengo la kujipatia Mkaa.
Amesema kuwa kitendo cha wananchi kukata miti hovyo ambao mpaka sasa umepelekea kuwepo kwa jangwa kwa baadhi ya maeneo na kusababisha ukosefu wa mvua kwa kipindi kirefu jambo ambalo ni hatari kwa kizazi kilichopo na kijacho.
Akitaja baadhi ya maeneo ambayo yanaongoza kwa ukataji wa miti kuwa ni tarafa ya Ndagalu ambayo inaogoza kukata miti hususan ya Matunda na Minyaa kwa lengo la kuni na mkaa amesema kuwa eneo hilo limegeuka jangwa hivyo mpaka sasa kuna kampeni ya upandaji wa miti na uelimishaji wa jamii kuhususiana na uwepo wa miti katika mazingira yao.
Dkt. Sengati ameyasema hayo wakati akizindua kiwanda cha kutengeneza mkaa mbadala kinachoitwa Kuni Smart cha Kisesa kinachotengeneza mkaa kwa takataka zinazotokana na mimea.
Naye Mkurugenzi wa Kiwanda hicho, Bw.Makachia amesema kujenga kwa kiwanda hicho eneo ambalo liko karibu na soko la Kisesa kutasadia pia kukusanya uchafu wa mimea unaotoka sokoni hapo lakini pia kuisaidia jamii kapunguza ukataji wa miti kwa lengo la kujipatia mkaa sambamba na ajira kwa vijana.
Bw. Makachia ameongeza kuwa mpaka sasa kiwanda hicho kimezalisha jumla ya tani 15 za mkaa ambao bei yake ni nafuu zaidi na unadumu kwa muda mrefu wakati wa kupika (Bandika Bandua) hivyo jamii ielimishwe kuhusiana na uwepo wa mkaa mbadala tofauti na ilivyozoeleka kwa mkaa unaotokana na miti.
Post A Comment: