WATANZANIA wamehimizwa
kujiunga kwa wingi na mfuko wa Bima ya Afya iliyoboreshwa ili wapate
vitambulisho vitakavyowasaidia kupata matibabu kwa mwaka mzima katika vituo vya
kutolea huduma za Afya ikiwemo na Hospitali za Rufaa.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Zainab
Telack akizindua Kampeni ya kuhamasisha wananchi kujiunga na mfuko wa Bima ya
Afya iliyoboreshwa mapema leo tarehe 16/07/2019, katika kijiji cha Ilobashi,
kata ya Masengwa, Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga, amesema Bima ya Afya
inawasaidia wananchi kuwa na uhakika wa matibabu kwa bei nafuu kwa mwaka mzima.
Amesema, wananchi wakiwa na
uhakika wa matibabu, maradhi yakiwakuta hawana fedha hawatakuwa na mawazo ya
kwenda kupiga ramli chonganishi kwa sababu tayari wana vitambulisho " Tusirudi huko ndugu zangu, kwenye
kupiga ramli" amesisitiza Telack.
Amewaasa wananchi ambao
vitambulisho vyao vimekwisha muda wake walipie tena kwa mwaka huu ili waendelee
kupata matibabu huku akiwakumbusha Waganga wafawidhi wa vituo vyote vya Afya
kuhakikisha dawa na vifaa vinakuwepo .
"Serikali
inataka Watanzania wote wanakuwa na Bima za Afya ili kuweza kutibiwa kwa
wakati, ubora na kwa bei nafuu, hakikisheni madirisha ya wagonjwa wa CHF
yanakuwepo na yanafanya kazi kama ilivyo kwa madirisha ya wazee" amesema Telack.
Naye Waziri wa Kilimo Japhet
Hasunga aliyeambatana na Mkuu wa Mkoa katika uzinduzi huo, amewasisitiza
wakulima wote kujiunga na mfuko wa Bima ya Afya mara tu watakapouza pamba ili
wawe na uhakika wa matibabu.
"Kazi
ya kilimo ina mchango mkubwa kwa pato la Taifa, asilimia 28.7 inatokana na
kilimo, hivyo siku hii ni muhimu sana kwa wakulima na mimi nasema, huwezi
kulima kama huna Afya nzuri" amesema Hasunga.
Wakiwahamasisha wananchi wengine
kujiunga na mfuko huu, William Gwisu na Salu Izengo ambao wameshajiunga kwa
muda mrefu, wameeleza mafanikio makubwa waliyoyapata kutokana na kujiunga
ikiwemo kuokoa fedha nyingi baada ya kulazimika kupewa rufaa kwenye Hospitali
kubwa.
Post A Comment: