Na  Ferdinand Shayo,Arusha.

Maelfu ya Watanzania wamefanya maombi ya kumuombea Raisi wa Tanzania Dr.John Pombe Magufuli pamoja na Viongozi wa serikali ili kuendeleza nguvu katika ujenzi wa Tanzania mpya ili kufukia uchumi wa Viwanda kama ilivyo ndoto ya Raisi.

Mji wa Arusha umefurika maelfu ya watu kutoka ndani na nje ya mkoa wa Arusha pamoja na mikoa ya Kilimanjaro,Manyara,Singida,Dodoma ambao wamekusanyika kwa ajili ya kuiombea serikali  na Watanzania kwa ujumla.

Mkurugenzi Msaidizi wa Redio  Safina ,Hellen Lema amesema kuwa maombi hayo yanalenga kuomba Mungu azidi kumpa nguvu Raisi Magufuli ili aweze kuwatumikia vyema Watanzania  na taifa la Tanzania lizidi kubarikiwa na kusonga mbele kiuchumi.

Mchungaji Pascal Thomas  amesema kuwa maombi hayo ya toba  dhidi ya maovu mbalimbali na kuhamasisha watu kumcha Mungu na kuondokana na uovu pamoja na kuwaombea viongozi.

Kwa upande wao wananchi Ester Mremi na  Joel Molel walioshiriki katika maombi hayo wameeleza umuhimu wa kuliombea taifa ili kuwa na muelelkeo chanya wa kimaendeleo na kufungua milango ya kiuchumi ili waweze kufanikiwa.

Share To:

Post A Comment: