Naibu
 Waziri wa Kilimo Mhe Omary Mgumba (Mb) akijibu swali bungeni leo tarehe
 10 Juni 2019 wakati wa mkutano wa kumi na tano wa Bunge la Bajeti 
Jijini Dodoma. 
Na Mathias Canal, Wizara ya Kilimo-Dodoma
Serikali
 imearifu kuwa inafanya utafiti na tathmini ya kina ya maji kujaa kwenye
 mashamba ya wakulima katika maeneo mbalimbali nchini.
Naibu
 Waziri wa Kilimo Mhe Omary Mgumba ameyasema hayo Bungeni Jijini Dodoma 
leo tarehe 10 Juni 2019 wakati akijibu swali la Mhe Yahaya Omary Massare
 wa Jimbo la Manyoni Magharibi aliyetaka kufahamu serikali ina mpango 
gani kuwasaidia wananchi kwa kuwajengea mifereji ya kuongoza maji 
yasiingie mashambani.
Mbunge
 huyo alisema kuwa Eneo la Mbuga linalozunguka Mji wa Itigi pamoja na 
kufaa kwa kilimo cha mazao mbalimbali kama Mahindi, Alizeti, Choroko na 
Dengu lakini eneo hili linajaa maji na kufanya kilimo kuwa kigumu.
Mhe
 Mgumba aliongeza kuwa Utafiti na tathmini hiyo itakapokamilika itakuja 
na mikakati na mapendekezo stahiki yatakayosaidia kutatua changamoto ya 
kujaa maji mashambani na kuwasaidia  wakulima wa eneo la mbuga linalozunguka mji wa Itigi ili kuongeza uzalishaji na tija.
Aliongeza kuwa eneo
 la mbuga linalozunguka mji wa Itigi limekuwa likijaa maji pale mvua 
zinapokuwa juu ya wastani ambapo historia inaonesha kuwa bonde hili 
lilijaa maji kipindi cha mwaka 1997/1998 wakati wa mvua za E-lnino na katika msimu wa 2015/2016 baada ya miaka tisa tangu wakati wa mvua za E-lnino mwaka 1997/98.
Aidha, alisema
 kuwa Serikali imelichukua suala la Mheshimiwa Mbunge na itatuma 
wataalam wa Kilimo na Tume ya Umwagiliaji kwa ajili ya kwenda kufanya 
utafiti na tathmini ya kina ya maji kujaa kwenye mashamba ya wakulima.
Utafiti
 na tathmini hiyo itakapokamilika itakuja na mikakati na mapendekezo 
stahiki yatakayosaidia kutatua changamoto ya kujaa maji mashambani na 
kuwasaidia  wakulima wa eneo la mbuga linalozunguka mji wa Itigi ili kuongeza uzalishaji na tija.
MWISHO
Post A Comment: