Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa amesema kuwa Pierre Liquid ataambatana na Timu ya Taifa, Taifa Stars katika fainali za AFCON zitakazofanyika nchini Misri.

Amemhakikishia hilo wakati akizungumza naye katika Viwanja vya Bunge Jijini Dodoma, ambapo Piere alikwenda kutembelea kwa mwaliko wa Spika wa Bunge, Job Ndugai.

Hayo yanajiri ikiwa zimepita siku kadhaa tangu Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda kutoa kauli ya kukosoa tabia ya watu kuvipa muitikio mkubwa vitu visivyo na msingi, akitolea mfano Mchekeshaji huyo aliyejizolea umaarufu kwenye vyombo vya habari pamoja na mitandao ya kijamii.

Katika hafla iliyoandaliwa na Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe, Jokate Mwegelo ambayo ilikuwa na malengo ya kutokomeza ziro katika wilaya hiyo, Makonda alisema kwamba watu wa 'hovyo' kama Pierre hawapaswi kupewa nafasi kwenye vyombo vya habari, hali iliyozua gumzo kubwa.
Share To:

msumbanews

Post A Comment: